Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala, akiongea na wadau wa sekta ya huduma wa msaada wa kisheria jijini Dar es Salaam jana wakati wa hafla/futari maalum iliyoandaliwa kumkaribisha rasmi katika nafasi ya uongozi wa juu wa shirika hilo. (Mpiga Picha Wetu)
Wadau wa sekta ya huduma ya Msaada wa kisheria wakifatilia mazungumzo wakati wa hafla/futari maalum iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana ya kumkaribisha rasmi Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Bi. Lulu Ng’wanakilala katika shirika hilo. (Mpiga Picha Wetu)
*****************************************
Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Legal Services Facility(LSF) Bi. Lulu Ng’wanakilala amesisitiza kuwa vipaombele vya shirika hilo ni kuhakikisha upatikanaji madhubuti wa huduma za msaada wa kisheria pamoja zinatolewa kwa wakati.
Lengo hili litawezekana kwa kutanua wigo wa kutoa huduma hizi muhimu ambazo zimewawezesha mpaka sasa mamilioni ya watanzani kupata haki zao tangu shirika hilo kuanzishwa mwaka 2011
Ng’wanakilala, amesema haya jana jijini Dar es saala wakati wa halfa ya Iftar iliyoandaliwa na LSF na kuwashirikisha wadau kutoka katika sekta mbalimbali , Serikali, wadau wa maendeleo , mashirika binafsi na mashirika yasiyo yakiserikali. Huku lengo hasa likiwa ni kumkaribisha na kumuwaga Afisa Mtendaji Mkuu Kees Groenendijk anayeondoka baada ya kuongoza shirika hilo tangu kuanzishwa kwake
“LSF imekuwa na mafanikio mengi ikiwemo mchango wake mkubwa kwa kushirikiana na wadau na Serikali katika kuwepo kwa sheria ya msaada wa kisheria yaani Legal Aid Act, 2017 ambayo inamufaa makubwa kwa mustakabali wa msaada wa kisheria kwa ujumla na si kwa LSF pekee.Agenda yetu kubwa sasa ni kuendelea kushirikiana na Wizara ya katiba na sheria katika utekelezaji wa sheria hiyo ili kuchochea uhakika, ufanisi na ubora wa huduma za msaada wa kisheria nchini”.Alisema
Akiongea kuhusu kazi kubwa iliyofanywa katika kila wilaya Tanzania na Zanzibar mpaka sasa, aliongeza” mkakati wetu mkubwa sasa ni kuangalia ni jinsi gani LSF itakuendelea kuwepo na kujenga zaidi kile kilichofanyika mpaka sasa. Lengo letu kubwa ni kuhakiksha sekta ya msadaa wa sheria
kupitia mtandao wetu mpana wa watoa huduma wa msaada wa kisheria “paralegal” unafikia kila jamii huku tukitilia mkazo uwezeshwaji wa wanawake , uwezeshwaji uchumi na kuondoa umaskini .
LSF tutafanya kazi kwa karibu na sekta mbalimbali hata zile ambazo hatukuwahi kushirikiana nazo kama vile sekta ya madini, kilimo, utalii na sekta binafsi kwa kuhakikisha paralegal wanatatua changamoto za kisheria zinazowakabili kwa namna moja au nyingine”.
LSF mpaka sasa ina jumla ya paralegal 4000 wanaotoa elimu juu ya maswala ya sheria na kutoa msaada wa kisheria kwa jamii nchi nzima. Mamia na maelfu ya wanawake, wanaume na Watoto wamefaidika na wanaendelea kufaidiaka na huduma hizi zinazosimamiwa na mashirika yanayotoa huduma za kisheria , paralegal na wadau washirika chini ya ufadhili wa DANIDA na DFID “ni matumaini yetu kwamba ushirikiano wetu kwa pamoja utawezesha LSF kutanua huduma zake na kuwafikia watu wengi zaidi na kuboresha Maisha yao kijamii na kiuchumi kwani huduma hizi za msaada wa kisheria ni bure”
Ms. Ng’wanakilala alianza kazi rasmi mwezi huu na ataongoza shirika lilodumu kwa miaka 8 kwa kuboresha mahusiano na serikali katika ngazi zote na kuwawezesha wananchi kupata haki zao kwa manufaa ya maendeleo yao na ya nchi kwa ujumla