Home Uncategorized GURU PLANET YATOA MAFUNZO YA MIFUKO MBADALA KWA WAJASILIAMALI

GURU PLANET YATOA MAFUNZO YA MIFUKO MBADALA KWA WAJASILIAMALI

0
Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
IKIWA zimebaki siku nne za katazo la serikali la kutokomeza mifuko ya platiki (rambo) vikundi mbalimbali vya ujasiriamali vimeanza kutumia fursa hiyo kwa kutengeneza mifuko ya karatasi.
Kampuni ya Guru Planet iliyopo Tabata jana iliwakusanya wajasiriamali kwa kutumia mikono waliweza kujifunza na kutengeneza mifuko ya karatasi kwa lengo la kusambaza madukani na sehemu za biashara.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Nickson Martin alisema lengo kuwafanya wajasiriamali kujiari lakini pia kuendana na kasi ya kuacha kutumia mifuko hiyo ya rambo.
“Hapa wajasiriamali wengi baada kuona tangazo wamejitokeza na kuanza kujifunza kutengeneza mifuko hiyo ambapo tunamshukuru Mungu kwa hilo  ila asilimia 90 ni akina mama na 10 akina baba  kwa pamoja wataanza kupata masoko yaliyowazunguka mitaani mwao ili kuweza kuendana na kasi ya katazo,”
“Hata hivyo naamini soko ni kubwa mno hivyo kila mtu ajira hii imeanzia pale alipo na naamini watafanikiwa,”alisema Martini.
Mwalimu wa mafunzo ya kutengeneza mifuko hiyo Bilhuda Mohamed alisema soko ni kubwa na huduma hiyo imeanzia kwa Dar es Salaam lakipi pia lengo kufika mikoani kote.
Wajasiriamali mbalimbali waliopata mafunzo hayo akiwemo Ester Sinduka (70) anasem alilisikia tangazo akiwa mkoani Mwanza na alipopata fursa kuja Dar es Salaam akaona ni vyema kujifunza ili akaweze kuwafundisha wajukuu zake jinsi ya kutengeneza mifuko hiyo.
Mafunzo hayo yameelewa kuwa na mwendelezo ambapo yatakuwa yanafanyika jumatatu,Alhamisi na jumamosi katika ofisi za Guru Tabata.

 Mkurugenzi wa Tasisi ya Guru Planet, Nikson Martn akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa mafunzo ya utengenezaji wa mifuko mbadala kwa Wanawake wajasiliamali wa Mkoa wa Dar es Salaam

 Mkurugenzi wa Tasisi ya Guru Planet, Nikson Martn akionyesha baadhi ya mifuko ambayo inatengenezwa na Wanawake Wajasiliamali

Mwalimu wa ujasiliamali kutoka Guru Planet,Bilhuda Mohamed, akionyesha baadhi ya vifaa vya kutengeneza mifuko mbadala

  Mwalimu wa ujasiliamali kutoka Guru Planet,Bilhuda Mohamed akiwa katika Mafunzo ya Vitendo na Wanafunzi na wanafunzi kutengeneza mifuko mbadala

Wajasiliamali wakijifunza kwa vitendo namana ya kutengeneza mifuko mbadala