Taasisi za elimu mkoani Dodoma zimeaswa kuzingatia malezi ya dini na kuzingatia misingi ya imani za wanafunzi wao pindi wanapokuwa shuleni.
Haya yamesemwa na Sheikh wa Msikiti wa Ipagala Ashiru ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa ya pamoja ya futari iliyoandaliwa na Shule za Fountain Gate Academy Dodoma.
Dennis Joel ni Mkuu wa Shule wa Fountain Gate Academy Azimio Sekondari Dodoma anasema utaratibu wa kuandaa futari kila mwaka na kuwakutanisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali, wazazi, wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali za mkoa awa Dodoma na majirani wanaoizunguka shule kwa ajili ya chakula cha pamoja.
Naye Rajab Said ni mwalimu mlezi wa wanafunzi wa Kiislam wa Fountain Gate Azimio Sekondari anabainisha jinsi utaratibu wa chakula cha pamoja unavyowajenga watoto kuwa na kasumba ya umoja hata katika taaluma.
Baadhi wa wanafunzi wakiwemo Safia Mikindo, Sabrina Mohamed, Layla Bakari, Athuman Nasoro na Rahma Juma wamepongeza utaratibu wa Fountain Gate Academy na kukueleza kuwa unawajenga kiimani na kuheshimu misingi ya dini ya Kiislam.
Zaidi ya watu 500 wameshiriki futari na kusikiliza tafsiri za aya mbalimbali, kusoma Quran, kuongoza swala na kutoa mawaidha katika viwanja vya Fountain Gate Azimio Sekondari Jijini Dodoma.