Home Mchanganyiko Wabunge Wanawake Dar, Watoa Ujumbe Mzito UWT

Wabunge Wanawake Dar, Watoa Ujumbe Mzito UWT

0

Wabunge wa viti maalum Mkoa wa Dar es salaam wamewataka wanawake wa umoja wa wanawake  CCM  (UWT) kuwa na umoja na mshikamano kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ili chama cha Mapinduzi kiweze Kupata ushindi wa kishindo.

Wabunge hao wametoa wito huowakati wa ziara yao mkoani Dar es salaam  kutembelea  wanachama  wa UWT,  ambapo wamesema iwapo wanachama hao watashirikiana ,kuacha makundi na kukisaidia chama, kitafanya vizuri katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge kazi na wenyeulemavu Mhe. Stella Ikupa , akizunguza  katika ziara hiyo,amewashukuru wanawake wa umoja huo kwa kuendelea kuwaungamkono wabunge wanawake viti Maalumu mkoa wa Dar es salaam na kuwa taka kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa Kufanyika mwakahuu.

Aidha ameitaka UWT  kuwahamasisha walevu kugombea nafasi katika uchaguzi huo na kuwaunga mkono kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi hakina ubauguzi.

“Nawashukuru  sana  kwa kuniamini katika uwakilishi nami nawakilisha walemavu wote nchini wakiwemo wa mkoa wa Dar es salaam,nilipo ingia Bungeni  swali langu la kwanza  lilikuwa kuhusu kupatiwa mikopo walemavu , nashukuru serikali ili kubali na sasa walemavu wanapatiwa  asilimia mbili ya mikopo ya halmashauri ” Alisema Ikupa

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angella  Kairuki, alisema  katika kujiandaa na uchaguzi Tathimini  inatakiwa Kufanyika na kikubwa zaidi   kufanyika maandalizi  ya kutosha na kusema kuwa  wasaliti wasipewe nafasi, pia  kuwatia moyo wanawake kugombea nafasi ili kufikia uwianno wa 50kwa 50 katika uwakilishi .

“Tuna shukuru sana kwa kuwa mmeendelea kumpongeza Rais Magufuli na kumuunga mkono katika shuguli zake za kuleta maendeleo ya nchi endeleeni na moyohuo” Alisema Kairuki.

Katika kujikwamua kiuchumi  Kairuki aliwataka wanawake hao kuchangamkia fursa za mikopo ya Halmashauri inayotolewa bila riba iweweze kujiendeleza kibiashara.

Kwaupande wake Mbunge wa viti Maalumu mkoa wa Dar es salaam,Mhe.Mariam Kisangi pamoja na kuwashukuru aliwataka akinamama hao  kwenda kuhamasisha wanawake kujiunga na chama cha Mapinduzi nakuhamasisha wanawake kuchukua nafasi za kugombea .

‘’Niwajibu wetu kama wabunge  kuwaelezea wanawake wenzetu waliotuchagua  mambo makubwa ya maendeleo abayo serikali imeyafanya  katika  Wilaya zetu , majimbo  na mkoa wetu kwa ujumla ,kunaujenzi wa daraja jipya la Salenda, Mradi wa DMDP umeboresha na kujenga barabara, ujenzi wa barabara ya  Morogoro eneo la kimara,na mambo mengine ya maendeleo ambayo serikali yetu ya Chama  Cha Mapinduzi  inaendelea kuyafanya’’Alisema Kisangi.

Naye Mwenyekiti wa umoja wa wanawake CCM (UWT)  Mkoa  wa Dar es salaam    ,Grace Chrispine Haule , aliwapongeza madiwani wa kwa uchapa kazi na utiifu kwa umoja huo pamoja na wabunge wanawake wa mkoa wa Dar es salaam pamoja na kuwa na majukumu mengi ya Kitaifa lakini wamekiheshimu  chama na wamekuwa wakiitika  wito kwa umoja huo.

“Kwa sasa tuna nafasi chache za madiwani wa viti Maalumu naomba tujitahidi tupate ushindi  ilituongeze viti sasa tunachofanya ni kuwafanya wanawake  waweze kujiamini  na tupate watakao gombea” Alisema

Pamoja na hayo Haule,  amempongeza Rais Dr  John Pombe magufuli  kwa kazi kubwa anayoifanya  akishirikiana na  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri mkuu Majaliwa,  kwa kiasi kikubwa wametimiza ahadi walizo ahidi na anaamini katika uchaguzi ujao CCM itaendelea kushinda kwa kishindo.

Nao baadhi ya wanachama wa umoja huo wa mewataka wabunge hao kushughulikia kero za miundombinu   ambayo imeharabika katika kipndi hiki cha mvu pamoja na  Umeme na maji kwa ni kunamaeneo  yanamahitaji huduma hizo.