Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA)Tike Mwambipile akikata keki pamoja na viongozi wengine wa Chama katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama ulifanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Chama hicho kinatimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA)Tike Mwambipile akikata vipande vya keki huku viongozi wengine wa Chama hicho wakishuhudia katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama ulifanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Chama hicho kinatimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka akizungumza katika mkutano wa mwaka wa Chama hicho ulioshirikisha wanachama wake ambao ni wanasheria wanawake, Mkutano huo umefanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
viongozi wengine wa Chama hicho wakiongoza Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama ulifanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Chama hicho kinatimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake.
Jaji Winfrida Koroso Mwanachama mwandamizi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA akizungumza katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama hicho uliofanyika jana kwenye hotel ya Serena jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA)Tike Mwambipile akifafanua jambo katika mkutano huo.
Meneja wa Benki ya (TIB) tawi la Samora Bw. Philip Pilla akitoa mada katika mkutano huo.
Mmoja wa wanachama wa chama hicho akiuliza swali katika mkutano huo.
Picha zikionyesha baadhi ya maofisa wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA).
Baadhi ya wanachama wa Chama hicho wakiwa katika mkutano huo.
Jaji wa Mahakamani Kuu ambaye pia ni mwanzilishi wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) , Joaquine De Mello amesema anafurahi kushuhudia chama hicho kikitimiza miaka 30 kikiwa kimepiga hatua kubwa na kinajiuza, hakijawahi kuyumba wala kutoka nje ya lengo la kuanzishwa kwake.
Alisema kipindi chote (TAWLA) kimekua mstari wa mbele kutumia taaluma ya kisheria kusaidia wanawake wasio na uwezo kupata msaada wa kisheria na haki zao ikiwa ni pamoja na kushughulika na masuala mbalimbali ya usalama barabarani.
Wanasheria wana faida kubwa, wanajua sheria, wanajua mikataba mbali mbali ya kisheria, lakini je wanatumiaje hizo nafasi zinapokuja?, lazima kujiulizaa kutafakari.
Wanawake ambao hawakupata nafasi ya kusoma, na wale wa ngazi za chini tunasema mfumo dume na kutojua sheria inayowakandamiza, sasa sisi tunaoijua tunaitumiaje, tunaonyesha mfano gani, tunafanya nini kama wanasheria.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWLA), Tike Mwambipile alisema chama hicho ambacho kinatimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake, kinaendelea kutoa misaada mbali mbali ya kisheria kwa wanawake na vijana kujua haki zao akitea mfano sheria ya ardhi ambayo wote wana haki sawa ya kumiliki.
“Miaka 30 ya (TAWLA) changamoto bado nyingi hasa kwa wanawake wanaokuja kutaka msaada wa kisheria, unamsaidia kwa nia njema lakini wengine wanamalizana kifamilia, mwisho tunaonekana wabaya, na kuonekana ndio tunamshawishi, kuchukua hatua.” alisema Mwambipile.