Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome akiangalia moja ya machapisho aliyoyakuta katika kituo cha msaada wa sheria cha NILIKO Cha mkoani Geita alipofanya ziara ya ukaguzi wa watoa msaada wa sheria mkoani humo.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome akipokea taarifa ya utoaji msaada wa sheria mkoani Geita kutoka kwa Mona ya taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa wananchi mkoani Geita.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome akizungumza na watoa msaada wa sheria mkoani Geita.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome katika picha ya pamoja na watoa msaada wa sheria kwa wananchi mkoani Geita
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome akiangalia moja ya machapisho aliyoyakuta katika kituo cha msaada wa sheria cha NILIKO Cha mkoani Geita alipofanya ziara ya ukaguzi wa watoa msaada wa sheria mkoani humo.Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome akipokea taarifa ya utoaji msaada wa sheria mkoani Geita kutoka kwa Mona ya taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa wananchi mkoani Geita.Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome akizungumza na watoa msaada wa sheria mkoani Geita.…………………Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome amewataka wasaidizi wa sheria nchini kufanya kazi zao kwa umakini kwa kuwa wanatambulika kwa mujibu wa Sheria ya Msaada wa Sheria No.1 ya 2017.Prof.Mchome ametoa kauli hiyo mjini Geita alipokutana na wasaidizi wa sheria wanaotoa huduma ya msaada wa sheria kwa wananchi mkoani Geita ambako yuko katika ziara ya kuangalia kama utoaji wa msaada wa sheria unaendana na matakwa ya Sheria ya Msaada wa Sheria ya mwaka 2017.“Sheria ya Msaada wa Sheria No.1 ya 2017 ilitungwa rasmi ili kuwatambua wasaidizi wa sheria, sasa ni jukumu lenu kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi kwani mnatambulika kisheria”,alisema Prof.Mchome.Amewataka kufanya kazi iliyokusudiwa na kutokujiingiza katika siasa na uanaharakati kwakuwa sheria ni msumeno na haiangalii itikadi, dini , jinsia ,sura wala rangi.Amesema utoaji sahihi wa msaada wa sheria kwa wananchi ukizingatiwa kikamilifu utatoa nafuu kwa wananchi na hivyo kupata jamii salama na kujiletea maendeleo.