Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Amos Makalla kulia akikabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu wa mkoa wa mpya Mh. Juma Zuberi Homela.
Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Amos Makalla aakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa mpya Mh. Juma Zuberi Homela pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa huo.
………………………………………………..
Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Amos Makalla amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu wa mkoa wa mpya wa Katavi Mh. Juma Zuberi Homela ambaye aliteuliwa na Rais Dkt, John Pombe Magufuli hivi karibuni.
Akizungumza katika makabidhiano hayo amesema amekitumikia Chama cha Mapinduzi (CCM)na Umoja wa vijana (UVCCM)kwa Muda mrefu na vipaji, uzoefu alionao atandelea kuwa Kada mwaminifu wa mstari wa Mbele wa Chama cha Mapinduzi
Amos Makalla amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumteua katika nafasi ya Ukuu wa Mkoa kwa miaka minne iliyopita akiitumikia mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya na Katavi katika uongozi Serikali ya awamu ya nne na ya tano
Amesema mwaka 2015 Alipokosa Ubunge ilitosha yeye kubaki mwananchi na mwana (CCM) tu huko Mvomero lakini Rais wa awamu ya nne Mhe Jakaya Kikwete alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na pia Rais Dkt. John Pombe Magufuli alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na baadaye Katavi.
Amewashukuru wananchi na viongozi wa ngazi zote dini na serikali kwa kumpa ushirikiano katika Kipindi cha miezi 10 alipokuwa mkuu wa mkoa wa Katavi na Amewaomba wananchi na viongozi wampe ushirikiano wa kutosha mkuu wa mkoa Mpya Juma Homela