Na Ahmed Mahmoud Longido
Jumuiya ya Afrika mashariki imetahadharisha wananchi kutokuwa na hofu wakati zoezi la mfano la magonjwa ya milipuko litakapofanyika katika mpaka wa nchi za Tanzania na Kenya eneo la namanga wilayani Longido Juni 11 hadi 14 mwaka huu.
Zoezi hili linakuja baada ya Agizo la Baraza la mawaziri wa Afya wa jumuiya hiyo la mwaka 2015 ambapo zoezi hili limelenga kuimarisha kiwango cha utayari na mwitikio kwa magonjwa ya mripuko katika ukanda wa Afrika mashariki(JAM\EAC)
Akitoa taarifa hiyo kwa Vyombo vya habari Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Jumuiya hiyo Dkt.Michael Katende anaeleza kuwa zoezi hilo la mfano litakalowashirikisha watendaji mbali mbali na askari linaweza kuzua taharuki kwa jamii hivyo wameona ni muhimu kutoa taarifa hii.
Anasema kuwa zoezi hilo la kuigiza kutokea kwa magonjwa ya mlipuko ni kuona jinsi gani mataifa ya jumuiya yamejipangaje kufikia na kutekeleza kwa viwango gani utoaji wa huduma pindi yanapotokea magonjwa hayo.
“Tunajua kuna muingiliano wa mataifa yetu katika Nyanja mbali mbali hivyo Afya jumuishi hinahitajika kuweza kujua changamoto za vifaa tiba ambazo hatujaweza kuwa nazo katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko yakiwemo Ebola,Homa ya bonde la Ufa na Homa ya manjano”
Anasema kuwa zoezi hilo la mfano wa kuigiza limelenga kuimarisha uwezo wa watu wote waishio kwenye mataifa hayo kutokana na muingiliano kwa lengo la jamii inayohusika kuweza kuzuia na kuweka Tathmini kwa kiwango gani tuna utayari na mwitikio wa mashiriki ya kimataifa kwa magonjwa ya kuambukiza.
Anasema zoezi hilo la kuigiza hali halisi ya ambapo kisa cha mripuko kinaweza kutokea wakati wowote zoezi hilo litwapa fursa washriki kubaini uwezo wao wa pamoja na mapungufu ili kuja na njia nzuri za kurekebisha mapungufu ya utendaji kazi yaliojitokeza wakati wa zoezi hilo.
Kwa Upande wake Mratibu wa Afya kutoka Shirika la maendeleo la Ujerumani (GIZ)anasema sio washiriki wote watakuwa namanga bali watahusika na zoezi wakiwa kwenye vituo vyao vya kawaida vya kazi katika miji ya Dar es salaam Nairobi Dodoma Arusha Longido na Kajiado na kwenye sehemu nyingine za mipaka
Anasema kuwa zoezi hilo litaratibiwa na kurugenzi ya jumuiya ya Afrika mashariki GIZ na WHO kwenye kituo cha pamoja cha mpakani(OSBP)
Asilimia kubwa ya magonjwa ya milipuko husambazwa kati ya wanyama na binadamu ambapo mripuko ya magonjwa hayo huathri shughuli za kibiashara Utalii Kilimo sambamba na maisha ya watu ambapo zoezi hili linakuja baada ya ugonjwa mlipuko kuikumba nchi ya CONGO DRC na kuambukiza watu takribani 1600 huku 1100 wakifariki dunia kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya ulimwenguni WHO.
Kutokana na taarifa ya nchi hiyo kukumbwa na ugonjwa wa Ebola ndio maana kuna umuhimu mkubwa wan chi zetu za Afrika Mashariki kuweza kujiandaa
Zoezi hili pia litafanyika kwenye mpaka wan chi za Uganda na Sudani Kusini hapo baadae kuweza kuimarisha watendaji kuweza kujiweka sawa kuyakabili magonjwa ya mlipuko pindi yanapotoke