RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo, kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Said Hassan Said.
WAZIRI wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim, akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yake kuazia mwezi julai 2018 hadi March 2019, katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, kushoto Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Said Hassan Said
WATENDAJI wa Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yao, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo.20-5-2019
NAIBU Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Hassan Ngwali akichangia wakati wa Mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar, uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo.20-5-2019, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Mhe. Said Hassan Said, akichangia wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Katiba na Sheria uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar
MWENYEKITI wa Tume ya Marekebisho ya Sheria Zanzibar Jaji Mshibe Ali Bakari, akichangia wakati wa hafla hiyo ya Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.(Picha na Ikulu)