Home Biashara Kampuni ya Halotel na Visa zimesaini mkataba wa kimkakati ambao utawezesha watumiaji...

Kampuni ya Halotel na Visa zimesaini mkataba wa kimkakati ambao utawezesha watumiaji wa Halopesa kufanya malipo kwa njia ya Visa kupitia simu zao

0

Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Nguyen Tien Dung kulia na Meneja wa Visa Tanzania Bi.Oliver Njoroge wakisaini mkataba wa kimkakati leo ambapo utawezesha wateja wa mtandao wa Halote kufanya malipo Salama kwa njia ya Visa kupitia simu zao za mkononi Hafla ya kusaini mkataba huo imefanyika makao makuu ya Kampuni ya Halotel Victoria jijini Dar es salaam.

Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Nguyen Tien Dung kulia akimsikiliza  Meneja wa Visa Tanzania Bi.Oliver Njoroge wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kusaini mkataba wa kimkakati leo, ambapo utawezesha watteja  wa mtandao wa Halotel kufanya malipo Salama kwa njia ya Visa kupitia simu zao za mkononi Hafla ya kusaini mkataba huo imefanyika makao makuu ya Kampuni ya Halotel Victoria jijini Dar es salaam.

…………………………………………………………..

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Tien Dung amesema kuwa ushirikiano kati ya kampuni hizo utawezesha watumiaji wa Halopesa kutumia huduma ya Visa kwenye simu zao kwa kufanya malipo ya bidhaa na kuweka pesa na kutoa kwa mawakala wa huduma ya Visa.

“Kwa ukuaji mkubwa wa idadi ya wateja wa Halotel na kuwa ni mtandao wa simu unaokuwa kwa haraka hapa Tanzania tangu tuanze kutoa huduma hapa nchini, tuna imani kwamba idadi ya watumiaji wa Halopesa pia itaendelea kuongezeka”. Amesema Dung.

Aidha Bw. Dung amesema Kuwait kwa sasa Halopesa in zaidi ya  mawakala 40,000 na kwamba nguvu ya huduma ya Visa inaipa Halopesa thamani na  uwezo zaidi wa kuwezesha wateja kufanya manunuzi kwa njia ya Visa kupitia simu zao.

“Kupitia ushirikiano huu, Halopesa inawapa wateja kulipa kwa muuzaji kwa kutumia msimbo (Code) iliyopo kwenye huduma ya Visa kwenye simu zao. Huduma hii ya Visa katika simu huwezesha wateja kupata fedha zao moja kwa moja kutoka katika akaunti zao za benki kupitia simu zao na kulipia bidhaa kwa wauzaji,kutuma pesa bila gharama yoyote, kuweka pesa au kutoa pesa kupitia wakala yeyote wa huduma ya visa”. Ameongeza Bw. Dung.

Kwa upande wake meneja wa huduma ya visa kwa Afrika Mashariki, Bw Kelvin Langley ameelezea kuwa ushirikiano huo unalenga zaidi katika kuunganisha watanzania kwenye huduma ya visa na kuleta usalama wa fedha zao kufanya malipo fanisi kwa huduma na bidhaa.

“Tunafarijika kwa ushirikiano huu kati yetu na kampuni muhimu ya huduma za mawasiliano ya simu kama Halotel. Ushirikiano wetu na Halotel utawafanya watanzania kulipa kwa kutumia Visa katika simu zao kupitia zaidi ya wachuuzi wapya 40,000. Pia itawasaidia kupanuka kwa wigo wa watanzania wanaotumia huduma za kifedha hapa nchini”. Amesema Bw. Langley.