Home Michezo JAFO AAGIZA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA...

JAFO AAGIZA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA VIWANJA VYA MICHEZO  VYA KISASA

0

Katibu Tawala Msaidizi(ELIMU) Mkoa wa Tabora Sussan Nussu akitoa maneno ya utanguzili jana wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca Cola Mkoani humo kwa mwaka 2019.

Baadhi ya wanafunzi kutoka shule za Sekondari za Manispaa ya Tabora wakiwa katika sherehe jana za  uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca Cola Mkoani humo kwa mwaka 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizundua jana mjini Tabora mashindano  ya Copa Coca Cola Mkoani humo kwa mwaka 2019 kwa niaba ya Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa .

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akisalamia na watoto waliohudhuria uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca Cola Mkoani humo kwa mwaka 2019 jana katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Picha na Tiganya Vincent

……………….

OFISI ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) imewaagiza Wakuu wa Mikoa , Makatibu wa Mikoa, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote kuhakikisha wanabainisha maeneo makubwa ambayo yanaweza kujengwa viwanja wa michezo vyenye hadhi ya kimataifa.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Waziri wa Nchi katika Ofisi  ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Selemani Jafo katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Copa Cola cola UMISETA mkoani Tabora.

Alisema hatua hiyo inalenga kukuza michezo mbalimbali hapa nchini na kuongeza ajira kwa vijana.

Jafo alisema sanjari na utengaji wa maeneo ya ujenzi wa viwanja aliaagiza maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya michezo  na burudani wahakikishe yasibadishwe matumizi na kuvamiwa.

Aidha Waziri huyo aliwaagiza  Wakuu wa Mikoa , Makatibu wa Mikoa, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kuhakikisha vipindi vya masomo ya michezo na masomo mengine ya burudani shukeni yafundishwa kwa nadharia na vitendo ili kuwajenga wanafunzi kuwa katika ari ya kukabiliana vema katika ushindani.

Aliongeza kuwa wanapaswa pia kuhakikisha kuwa kila Shule ina viwanja vya michezo vyenye vipimo sahihi vinavyotakiwa na kusimamia Sheria ya Elimu inayotaka Shule inaposajiliwa lazima iwe na eneo la viwanja vya michezo.

Jafo pia aliagiza kuwa Shule zilizoteuliwa kuwa na mchepuo wa michezo ziimarishwe na walimu wake wasihamishwe.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo amewataka viongozi mbalimbali wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanatekeleza agizo la Mheshimiwa Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan la kuhimiza mchakamchaka kwa wanafunzi na wananchi kufanya mazoezi kuepuka magonjwa yasiyoambukiza.