Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Anthony Mavunde ameitaka mifuko ya Uwezeshwaji Wananchi Kiuchumi Nchini kuunga mkono jitihada za Vijana walioamua kujiajiri kwa kuwawezesha mitaji ili waweze kufikia malengo yao.
Mavunde ameyasema hayo leo Wilayani Kibaha alipomtembelea Kijana Mjasiriamali Ndg Robert Samson Lugara katika shamba lake la kuku ili kuangalia maendeleo ya ujezi wa miumbo mbinu ya ufugaji wa kuku na pia kusikiliza changamoto zinazowakabili vijana wanaojiajiri.
“Nimefurahishwa sana na uwekezaji huu mkubwa wa shamba la kuku 20,000 ambao utatoa Ajira kwa zaidi ya Vijana 100.Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Vijana ili kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba katika kujiajiri,lakini pia niwatake Vijana wengine wenye nia na mawazo ya kujiajiri kutumia mifuko ya uwezeshwaji wananchi kuongeza mitaji yao katika kufikia malengo yao”Alisema Mavunde
Akitoa maelezo yake ya awali, Ndg Robert Samson Lugara amebainisha kwamba lengo kuu la kufanya ufugaji huo ni kuhakikisha anaunga mkono juhudi za serikali kwenye kutatua tatizo la Ajira kwa Vijana na kuw mstari wa mbele kushiriki katika uchumi wa Viwanda kwa vitendo,ambapo pia amemshukuru Naibu Waziri Mavunde kwa kumtembelea shambani hapo na kumtia moyo na kusikiliza changamoto zinazomkabili kubwa ikiwa ni ya miundombinu ya barabara kuingia shambani ambayo ameahidi kuifikisha mamlaka husika kwa utatuzi.