Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho Bi. Agnes Robert.
………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
KAIMU Mkurugenzi mkuu wa Kijiji cha Makumbusho ya Taifa Agnes Robart amesema ili kuendena na mabadiliko ya teknolojia wao kama Makumbusho ya Taifa wamejipanga kikamilifu kutumia mitandao mbalimbali ili kuendelea kuitangaza Makumbusho hiyo.
Amesema wamejipanga vizuri huku akiwataka wazazi kuhamasika kutembelea Makumbusho kwa lengo la kuendelea kurithi tamaduni mbalimbali hususani za kale.
Agnes ameyasema hayo leo hii jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari katika kilele cha siku ya Makumbusho Duniani ambapo amesema lazima tuendelee kuenzi tamaduni za asili nchini.
” Hii Makumbusho inaazimishwa kila ifikapo Mei 18 kila mwaka na lengo nikujifunza Mila na desturi ambazo wazee wetu wametuachia “amesema Agnes
Akizungumzia Makumbusho ya Taifa amesema Makumbusho hiyo imeandaa tamasha la mama na mwana ambalo linalenga wazazi na watoto kujifunza juu ya kurithi wao.
Pia katika kauli mbiu ya mwaka huu ni Makumbusho ni” kitovu cha utamaduni :Hatma ya mila na Desturi ” na katika jijini cha Makumbusho wanafanya mambo mengi.
Mkurugenzi Agnes amesema katika kijiji cha Makumbusho vitu vingi vya kiutamaduni ikiwa pamoja nyumba za makabila mbalimbali kama vile Wangoni,wasukuma,wakwere,
Pia amesema kuna shughuli mbalimbali za kitamaduni zinafanywa kama vile vyakula vya asili ,maharagwe yanayoungwa kwa nazi,mboga za majani,ugari wa muhogo,na mambo mengine mbalimbali.
Pia ametoa wito kwa watanzania kujitokeza katika Makumbusho hayo kwa lengo la kuona mambo mbalimbali yaliyopo ndani ya kijiji hicho cha Makumbusho nakwamba kufanya hivyo ni kuendelea kulinda na kujifunza utamaduni wa Taifa.