Home Burudani MABRICHI: MTAYARISHAJI WA BONGO FLEVA ANAVYOKUJA KIVINGINE

MABRICHI: MTAYARISHAJI WA BONGO FLEVA ANAVYOKUJA KIVINGINE

0

NA EMMANUEL MBATILO

Mtayarisha wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Rahim Mataja ameamua kujichanganyai katika tasnia ya Uchekeshaji ambapo ameamua kuonyesha kipaji kingine alichonacho nje ya muziki.

Mtayarishaji huyo ambaye alitamba hapo mwanzo baada ya kufanya kazi na wasanii wakubwa wa hapa nchini na nje ya nchi amesema ameamua kufanya uchekeshaji lakini hatoacha kuendelea kutayarisha muziki kwani ni kazi ambayo anaipenda na anaona anafanya vizuri.

“Nimeamua kuonyesha kipaji changu cha uchekeshaji ili niweze kulipaisha vizuri jina langu wengi walikuwa hawanifahamu, walikuwa wanauliza hivi Cat P ndo nani, walishindwa kunifahamu licha kazi zangu nyingi kujulikana”. Amesema mabrichi.