Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli Rweyemamu akitoa elimu ya shinikizo la juu la damu kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu Duniani.
Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Maria Semlongo akitoa elimu ya lishe bora kwa afya ya moyo kwa ndugu wa wagonjwa wanaotibiwa katika taasisi hiyo ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu Duniani. Katika kuadhimisha siku hiyo JKCI ilifanya upimaji kwa ndugu waliowasindikiza wagonjwa ambapo asilimia 39 walikutwa na shinikizo la juu la damu bila ya kujifahamu.
Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akizungumza na mmoja wa mzazi ambaye mtoto wake anatibiwa katika Taasisi hiyo kuhusu lishe bora kwa watoto wakati wa maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu Duniani iliyogfanyika leo Jijini Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku hiyo JKCI ilifanya upimaji kwa ndugu wanaosindikiza wagonjwa kwa kuwapima viashiria vya magonjwa ya moyoambavyo ni urefu, uzito na shinikizo la damu.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Regan Valerian akizungumza na ndugu wa mgonjwa anayetibiwa katika Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu Duniani iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku hiyo wagonjwa walipewa elimu na ndugu waliosindikiza walifanyiwa vipimo vya viashiria vya magonjwa ya moyo bila malipo ambapo asilimia 39 walikutwa na shinikizo la juu la damu bila ya kufahamu kuwa wanalo.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Steven Charles akimpima urefu na uzito ndugu wa mgonjwa anayetibiwa katika Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu Duniani iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha na – JKCI