Watalii kutoka nchini China wakipata huduma ya kubadirisha fedha za kigeni katika Benki ya NMB kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro muda mfupi baada ya watalii Zaidi ya 345 kuwasili nchini kutokea China juzi jioni. Benki ya NMB ni wadau wa ugeni huu na imedhamini mikutano yao wakiwa hapa nchini.
Watalii kutoka nchini China wakiondoka kwenye dirisha la Benki ya NMB baada ya kubadirisha fedha za kigeni kupitia Benki hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro muda mfupi baada ya watalii Zaidi ya 345 waliowasili nchini kutokea China juzi jioni. Benki ya NMB ni wadau wa ugeni huu na imedhamini mikutano yao wakiwa hapa nchini.
Watalii kutoka nchini China wakiondoka kwenye dirisha la Benki ya NMB baada ya kubadirisha fedha za kigeni kupitia Benki hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro muda mfupi baada ya watalii Zaidi ya 345 waliowasili nchini kutokea China juzi jioni. Benki ya NMB ni wadau wa ugeni huu na imedhamini mikutano yao wakiwa hapa nchini.
……………………………………………………………..
Katika kuhakikisha hali ya uchumi inazidi kuimarika kupitia sekta ya utalii, Tanzania imepokea watalii Zaidi ya 340 kutoka nchini China ikiwa ni wiki kadhaa toka watalii zaidi ya 1000 kuwasili nchini kutoka nchini Islael.
Watalii hao kutoka nchini China walifika juzi jioni na kupokelewa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania – Majaliwa Kasim Majaliwa, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kingwangala, Mwenyekiti wa bodi ya Utalii Thomas Mihayo na uongozi mzima wa Benk ya NMB ambao ndio wadhamini wa ugeni huo.
Katika hatua nyingine Waziri mkuu aliipongeza sana kampuni ya china ya TASH-ROAD INTERNATIONAL GROUP iliyoko chini ya M/kiti He Lei Hiu kwa upendo wa dhati aliouonyesha wa kukubali kuingia makubaliano na nchi ya Tanzania kwa kuwaleta watalii hao zaidi ya 300 ambapo itakuwa ni mwanzo mzuri wa kuendelea kujitanua zaidi na kuutangaza utalii katika anga zote za kimataifa.
Meneja wa NMB anayeshughulikia dawati la China – Agness Mulolele alisema kuwa, Benki ya NMB inaunga mkono jitihada za serikali katika kuendelea na kukuza utalii nchini hivyo wameamua kusogeza huduma karibu ili kuweza kuwahudumia watalii wote katika huduma zote za kifedha.
Kama ambavyo unatuona leo tumevalia sare zetu kuonyesha ni jinsi gani tumeamua kuja kutoa huduma zetu hapa kama sehemu ya kusaidia nchi yetu kufikia malengo makubwa ya maendeleo ikiwemo kuweka mazingira bora kwa watalii wanapotembelea nchini ili waweze kupata huduma bora za kibenki ikiwemo kubadirisha fedha za kigeni.
“Mkoa wowote watakao enda, wilaya yoyote watakayoenda, wajue sisi tupo na tutawahudumia bila tatizo lolote kwani tunapatikana katika wilaya zote nchini huku tukiwa na matawi 229 nchini kote.” Alisema Bi Mulolele
“Kama unavyofaham ndani ya watalii hawa kuna wafanyabiashara, wandishi wa habari, wamiliki wa makampuni ambao watahitaji huduma zetu na ndio maana tumeamua kuwa miongoni mwa watu wanaokuja kuwapokea” aliongeza Bi Mulolele
Wageni hawa kutoka china wametokea katika majimbo mawili ambayo ni HEJIAN’G na SHAN’GAI ambao jumla walikuwa ni 345 huku ndani yao wakiwemo wandishi wa habari 40, wamiliki wa makampuni 20 na wawekezaji 50 na wengine ambao wanatokea katika bodi tofauti za utalii nchini China, watakuwa nchini kwa siku nane kisha wataondoka kwenda nchi nyingine ambapo watakuwa katika zoezi lao zima la kuzizuru nchi tatu barani Afrika.