KAMPENI YA MPANGO HARAKISHI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU WILAYANI TUNDURU YAWAFIKIWA WAFUGAJI
Baadhi ya Wananchi wa jamii ya Wafugaji wa kitonngoji cha Chilundundu kata ya Misechela wakisubiri kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya Ugonjwa wa kifua kikuu kutoka Wataalam wa kitengo cha kifua Kikuu na Ukoma Hospitali ya Wilaya Tunduru. Wataalam kutoka kitengo cha Kifua Kikuu na Ukoma Hospitali ya wilaya Tunduru wakitoa huduma ya uchunguzi kwa watu wa jamii ya Wafugaji wanaofanya shughuli zao katika kitongoji cha Chilundundu kata ya Misechela wilayani humo. ……………………… Na Muhidin Amri, Tunduru WIZARA ya Afya kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma imesema,kampeni ya mpango harakishi wa uibuaji Wagonjwa wa Kifua Kikuu itawafikia watu wote waliobainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo ambao hawakufikiwa mwaka 2024. Watu hao,wataanzishiwa Dawa haraka kwa ajili ya kuzuia uwezekano wa kuambukiza watu wengine ili kuifanya Tanzania kuwa nchi salama bila kuwa na watu walioambukizwa ugonjwa wa kifua kikuu ifikapo mwaka 2030. Hayo…