Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichoshirikisha wawekezaji wa makampuni 13 kutoka Austria na Ofisi ya Mkuu wa mkoa, Kituo cha uwekezaji na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, waliokuja kwa lengo la kutafuta maeneo ya uwekezaji.
Washiriki wa kikao kilichoshirikisha wawekezaji wa makampuni 13 kutoka Austria na Ofisi ya Mkuu wa mkoa, Kituo cha uwekezaji na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, waliokuja kwa lengo la kutafuta maeneo ya uwekezaji, wakifuatilia mawasilisho katika kikao hicho.
Baadhi ya wawekezaji wa makampuni 13 kutoka Austria wakifuatilia maada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kikao kilichoshirikisha wawekezaji hao na Ofisi ya Mkuu wa mkoa, Kituo cha uwekezaji na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, waliokuja kwa lengo la kutafuta maeneo ya uwekezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akiagana na jopo la wawekezaji wa makampuni 13 kutoka nchini Austria mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichoshirikisha wawekezaji hao na Ofisi ya Mkuu wa mkoa, Kituo cha uwekezaji na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, waliokuja kwa lengo la kutafuta maeneo ya uwekezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge wa tano kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na jopo la wawekezaji wa makampuni 13 kutoka nchini Austria, Viongozi kutoka jiji la Dodoma, na kituo cha uwekezaji mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichoshirikisha wawekezaji hao na Ofisi ya Mkuu wa mkoa, Kituo cha uwekezaji na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, waliokuja kwa lengo la kutafuta maeneo ya uwekezaji.
…………………………………………………………………………………………
Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.
Jopo la wawekezaji wa makampuni mbalimbali kumi na tatu (13) kutoka nchini Austria wamewasili jijini Dodoma kwa ajili ya kutafuta maeneo ya uwekezaji katika sekta za usafirishaji, elimu, kilimo, afya na ujenzi wa miondombinu.
Akizungumza mara baada ya kufanya kikao kati ya wawekezaji hao, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kituo cha uwekezaji na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amesema wamefanya mawasilisho kwa pande zote mbili huku jiji la Dodoma wakionyesha maeneo muhimu na fulsa zilizopo.
“Leo tumepokea ugeni mzito kutoka Austria wakitafuta maeneo ya uwekezaji tumepata mda wa kila mtu kuwasilisha kwa upande wake wenyewe wakituonyesha maeneo watakayowekeza na wenzetu jiji wakaonyesha fulsa zilizopo pamoja na maeneo ya kuwekeza” amesema Dkt Mahenge.
Amebainisha kuwa wawekezaji hao wameonyesha nia ya kuwekeza katika maeneo ya usafirishaji, elimu, kwenye kilimo, afya na ujenzi wa miondombinu jambo ambalo ni muhimu sana katika mkoa wa Dodoma hasa ukizingatia katika wakati huu tunajenga makao makuu.
“Uzuri ni kwamba hata wao walipokuwa wanakuja walifahamu kuwa Dodoma ni makao makuu kwahiyo hata fulsa wanazotaka kuwekeza zimelenga katika ujenzi wa miondombinu na huduma za kijamii katika mkoa wetu” amesema.
Amesema Dodoma ni jiji linalojengwa karne ya 21 kwamba ni jiji linalojengwa kisasa na linalopangiliwa vizuri kuungwa mkono na wawekezaji kama hao ni muhimu katika kuwekea miondombinu sawa na huduma za kijamii zinatakiwa kuwa za uhakika katika sekta zote.
“Hapa Dodoma tunahospitali chache sana kuna huduma ukizikosa katika hospitali ya Benjamini Mkapa inabidi utoke nje ya mkoa kufuata huduma hizo, kiujumla hospital ni chache sana lakini un apopata wawekezaji kama hawa tunaamini tutapata huduma za uhakika na kuweka viwanda vya dawa” amesema.
Amesema miongoni mwa fulsa nyingine wanazotafuta wawekezaji hao ni usafirishaji hasa wa treni zinazotumia nishati ya gasi na ni gharama nafuu ukilinganisha na usafiri wa sasa unaotumia mafuta ambayo sio rafiki kwa mazingira.
Amesema amewaeleza upatikanaji wa zao pekee la zabibu linalopatikana katika mkoa wa Dodoma pekee pia hata bidhaa itokanayo na zao hilo ni nzuri ukilinganisha na zinazozalishwa katika maeneo mengine zinakopatikana bidhaa hizo.
“Hapa kwetu nimewaeleza kuna zao la zabibu ambalo ni tofauti na kwingine yani inaradha ya kipekee kabisa, kwahiyo nimewakaribisha kuona namna ya kuwekeza katika viwanda vinavyozalisha bidhaa za zabibu” amesema.
Kwa upande wake Mchumi wa Jiji la Dodoma bwana Shabani Juma wakati akiwasilisha vipaombele vilivyopo katika jiji amesema jiji la Dodoma limepima viwanja sambamba na kutenga maeneo ya uwekezaji na makazi katika eneo la uwekezaji ambapo pia limeunganishwa na huduma zote za kijamii.