Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge akisalimiana na Mtendaji mkuu wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah wakati alipowasili kwenye uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania leo jijini Dar, Maadhimishi hayo yanatarajiwa kufanyika katika vituo vyote vya Kampuni ya Puma Duniani, kwa hapa nchini Tanzania yatafanyika katika mikoa yote ambayo ina vituo vya Puma Energy kuanzia Novemba 30, 2020 hadi Desemba 4, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania leo jijini Dar, Maadhimishi hayo yanatarajiwa kufanyika katika vituo vyote vya Kampuni ya Puma Duniani, kwa hapa nchini Tanzania yatafanyika katika mikoa yote ambayo ina vituo vya Puma Energy kuanzia Novemba 30, 2020 hadi Desemba 4, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge akijaza mafuta kwenye gari huku Mtendaji mkuu wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah akipiga makofi wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania leo jijini Dar. Maadhimishi hayo yanatarajiwa kufanyika katika vituo vyote vya Kampuni ya Puma Duniani, kwa hapa nchini Tanzania yatafanyika katika mikoa yote ambayo ina vituo vya Puma Energy kuanzia Novemba 30, 2020 hadi Desemba 4, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge akimsikiliza Mtendaji mkuu wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania leo jijini Dar,anaeshuhudia kati ni Mkuu wa Rasilimali watu Afrika na Mashariki ya Kati Kampuni ya Mafuta ya Puma,Loveness Hoyange. Maadhimishi hayo yanatarajiwa kufanyika katika vituo vyote vya Kampuni ya Puma Duniani, kwa hapa nchini Tanzania yatafanyika katika mikoa yote ambayo ina vituo vya Puma Energy kuanzia Novemba 30, 2020 hadi Desemba 4, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge akijaza mafuta katika moja ya pikipiki huku Mtendaji mkuu wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah kushoto akifurahia wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania leo jijini Dar,Maadhimishi hayo yanatarajiwa kufanyika katika vituo vyote vya Kampuni ya Puma Duniani, kwa hapa nchini Tanzania yatafanyika katika mikoa yote ambayo ina vituo vya Puma Energy kuanzia Novemba 30, 2020 hadi Desemba 4, 2020.
Mtendaji mkuu wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah akifurahia wiki ya huduma kwa wateja pamoja na waenesha bodaboda wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania leo jijini Dar,Maadhimishi hayo yanatarajiwa kufanyika katika vituo vyote vya Kampuni ya Puma Duniani, kwa hapa nchini Tanzania yatafanyika katika mikoa yote ambayo ina vituo vya Puma Energy kuanzia Novemba 30, 2020 hadi Desemba 4, 2020.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye kituo cha mafuta cha Puma Energy jijini Dar leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge akizungumza huku Mtendaji mkuu wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah akimsikiliza wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania leo jijini Dar,
………………………………………….
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ameviagiza vituo vya uuzaji wa Mafuta kuhakikisha wanazingatia masharti ya leseni za biashara hiyo ikiwa ni pamoja na ubora wa Mafuta, tahadhari za kiusalama kwenye vituo, ubora wa huduma na kuepuka kupandisha gharama za Mafuta kinyume na utaratibu.
RC Kunenge ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja kwa vituo vya Mafuta vya Puma Energy ambapo ametoa wito kwa wafanyakazi wanaotoa huduma kuwa na mahusiano mazuri na wateja.
Aidha RC Kunenge amesema sekta ya Mafuta ni muhimu Sana Katika kurahisisha shughuli za kijamii na uchumi hivyo amewahimiza kuzingatia huduma Bora
Kunenge amevutiwa na utendaji kazi wa kampuni ya mafuta Puma Energy kutokana na kujali wateja wake na huduma bora wanazozitoa.
Akizungumza wakati wa wiki ya huduma kwa wateja inayoendeshwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo, Kunenge alisema aina ya biashara wanayoifanya inahitaji ubunifu na ushindani mkubwa kwa kuwa inafanywa na kampuni nyingi.
Aidha, kampuni hiyo ambayo inamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 50 imeonyesha uwezo mkubwa wa kutoa huduma za viwango vya juu kwa kipindi chote iliyokuwepo nchini.
“Navutiwa namna mnavyokuwa karibu na wateja, pia nimesikia mmejipanga kuimarisha huduma zenu katika wiki hii ya huduma kwa wateja, mara nyingi wateja wanapenda kuangalia vigezo kama bei, ubora wa bidhaa na taswira yenu ikoje mbele ya jamii.
“Vingine wanavyozingatia wateja ni usalama wa vyombo vyao, aina ya wafanyakazi mlio nao na mara nyingi wanapenda kulinganisha. Kwa kuwa kampuni hii ipo maeneo mengi barani Afrika wanataka kuona huduma aliyoipata nje ya Tanzania ilingane vilevile,” alisema Kunenge.
Awali akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Kituo cha mafuta Puma Upanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah alisema maadhimisho ya mwaka huu yanatokana na mafanikio makubwa waliyoyapata mwaka jana mwezi Disemba.
“Maadhimisho yatafanyika katika vituo vyote vya Kampuni ya Puma duniani, kwa Tanzania tutafanya katika mikoa yote ambayo ina vituo vya Puma Energy kuanzia Novemba 30, 2020 hadi Disemba 4, 2020.