MSIMAMIZI wa uchaguzi jimbo la Ubungo, Beatrice Dominic, amemtangaza Profesa Kitila Mkumbo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi katika jimbo hilo.
Beatrice amesema idadi ya ya wapiga kura waliojiandikisha ilikuwa 349,057 na waliojitokeza kupiga kura ni 89,656 ambapo kura halali ni 88,274 na zilizoharibika ni 1,382.
Msimamizi huyo amesema Prf.Mkumbo amepata kura 63,221 akifuatiwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniphace Jacob, aliyepata kura 20,620 huku mgombea wa ACT Wazalendo, Renatus Pamba, akipata kura 2,188.