Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Minjingu akitokea Karatu wilayani karatu mkoani Arusha akiwa njiani kuelekea Babati mkoani Manyara kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni za CCM leo Jumapili Oktoba 25, 2020.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-MINJINGU)
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Minjingu akitokea Karatu wilayani karatu mkoani Arusha akiwa njiani kuelekea Babati mkoani Manyara kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni za CCM leo Jumapili Oktoba 25, 2020.
Mbunge mteule wa jimbo la Babati Vijijini Ndugu Daniel Sillo akimuombea kura Rais Dk. John Pombe Magufuli katika eneo la Minjingu wilayani Babati mkoani Manyara.
Baadhi ya akina mama wa kimasai wakifurahia Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati alipozungumza na wananchi wa Minjingu akiwa njiani kuelekea babati.
Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Arusha wakimsikiliza Rais Dk. John Pombe Magufuli alipozungumza na wananchi wa Minjingu akiwa njiani kuelekea Babati.
Baadhi ya viongozi wa serikali wakiwa katika mapokezi hayo ya Rais Dk. John Pombe Magufuli eneo la Minjingu.
Mkuu wa mkoa wa Manyara Josephati Mkirikiti kulia na Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta wakimsikiliza Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati akizungumza na wananchi wa Minjinge.
Picha zikionesha baadhi ya viongozi wa mkoa wa Manyara wakiwa katika mapokezi hayo.
Picha mbalimbali zikionesha wananchi aliojitokeza katika mapokezi ya mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk John Pombe Magufuli eneo la Minjingu.