Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Korogwe katika mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Korogwe mkoani Tanga Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia Wananchi wa Korogwe mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Mkutano wa Kampeni
Sehemu ya Wananchi wa Korogwe waliohudhuria mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Korogwe.
………………………………………………………………………………..
Na.John Bukuku,Tanga
MGOMBEA urais wa CCM Dkt.John Magufuli ameendelea kuchanja mbuga kwa kufanya Kampeni zake katika wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga huku akiendelea kuomba ridhaa ya wana CCM, na wananchi kumchagua kuwa Rais na kuchagua wabunge na madiwani wa CCM.
Akiwa katika Mkutano huo,Dkt.Magufuli ameahidi kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupandisha mishahara kwa watumishi iwapo atapewa ridhaa hiyo.
“Miaka mitano iliyopita, tumeajiri watumishi 74,000, tumeimarisha uchumi wetu, sasa miaka mitano ijayo tutakuwa na jukumu la kuongeza mishahara, huwezi kupandisha mishahara wakati huna uchumi, wengine wanazungumza tu hawajawahi kutawala, hata kujenga ofisi za chama zimewashinda”amesisitiza
Aidha Dkt.Magufuli ameendelea kuwasisitiza wananchi kuendelea kutunza amani wakati huu wa uchaguzi kwani nchi ikivurugika Taifa litaingia kwenye matatizo.
Katika miaka mitano iliyopita tumetekeleza miradi 64 ya maji katika Mkoa wa Tanga, huku 54 ikiwa vijijini na 10 iko mjini, miongoni mwake ni mradi wa Pongwe, Muheza, tumetekeleza miradi 64 ya maji katika Mkoa wa Tanga, huku 54 ikiwa vijijini na 10 iko mjini, miongoni mwake ni mradi wa Pongwe, Muheza.
Hivyo tumejipanga kufanya makubwa katika Mkoa wa Tanga ,Mkoa huu una historia tangu enzi za ukoloni ,huu ni mkoa ambao Wajerumani walijenga Shule ya kwanza na kupata neno Shule Jiji la Tanga ni miongoni mwa majiji ya kwanza kabisa nchini.
Hata hivyo Dkt.Magufuli amesema kuwa uwepo wa ujenzi wa bomba la mafuta ambalo litatoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga litafungua fursa nyingine za kiuchumi kwa wananchi kwani kuna watu watafanya kazi katika ujenzi, wenye gesti watapata wageni, mama lishe watauza chakula pamoja na shughuli nyingine za kimaendeleo zitafanyika na kuwa tayari fidia ya Sh.bilioni tatu zimeanza kulipwa kwa wananchi ambao mradi utawapitia.