Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa anatoa salamu za  pole kwa familia, ndugu jamaa na marafiki kufuatia kifo cha Mtendaji Mkuu  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Prof. Damian M. Gabagambi aliyefariki  dunia leo tarehe 20 Oktoba, 2020 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini  Dar es salaam. 

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya msiba wa Mtendaji  Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Natambua mchango wake  mkubwa katika kuendeleza Sekta ya Viwanda na Biashara hapa  nchini”. 

Mhe. Bashungwa ametoa pole kwa menejimenti na wafanyakazi wa Shirika la  Maendeleo la Taifa (NDC) na wadau wote wa viwanda na biashara hapa nchini. 

“Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe”