Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida (Mandewa) wakiangalia vipeperushi vya Shirika hilo vinavyoelekeza kanuni za uchaguzi.
Afisa Utawala wa Shirika hilo, Loveness John akimkabidhi vipeperushi hivyo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Senge, Benjamin Mayengera kwa niaba ya walimu wa shule hiyo.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Women Wake-up (WOWAP) Issah Shayo, akimkabidhi vipeperushi hivyo Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Sabasaba, Grace Benjamini kwa niaba ya walimu wa shule hiyo.
Afisa Utawala wa Shirika hilo, Loveness John, akitoa Elimu ya Uraia ya Mpiga Kura kwa Walimu wa Shule ya Msingi Sabasaba.
Watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mwalimu Angela John wa Shule ya Msingi Sabasaba, akiuliza swali kwaWatendaji wa WOWAP wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Women Wake-up (WOWAP) Issah Shayo, akimkabidhi vipeperushi hivyo Mwakilishi wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Basil Pesambili kwa niaba ya wenzake.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Women Wake-up (WOWAP) Issah Shayo, akimkabidhi vipeperushi hivyo Msaidizi wa Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel, Remmy Aloyce kwa niaba ya wenzake. Kulia ni Afisa Utawala wa WOWAP, Loveness John.
Afisa Utawala wa WOWAP, Loveness John, akitoa Elimu ya Uraia ya Mpiga Kura kwa Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida (Mandewa)
Godwin Myovela na Dotto Mwaibale, Singida.
SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Women Wake-Up (WOWAP) limekumbusha
jamii kuhakikisha ifikapo Oktoba 28 mwaka huu kila mwenye sifa ya kupiga kura ajitokeze
na kadi yake ya kupigia kura katika kituo alichojiandikisha ili kutimiza haki
yake ya msingi ya kikatiba
Aidha, shirika hilo limesisitiza umuhimu wa kila mtanzania
kuzingatia misingi ya amani na utulivu wakati mchakato huo ukiendelea, ikiwemo kufika
mapema kituoni kupiga kura na kuondoka kuendelea na majukumu mengine kwa mujibu
wa sheria za uchaguzi, ili kuepusha madhara au viashiria vya uvunjifu wa amani
vinavyoweza kujitokeza
Afisa Utawala wa WOWAP, Loveness John aliyasema hayo kwa
nyakati tofauti jana wakati akielimisha na
kukumbusha jamii mkoani hapa juu ya namna bora ya kufanikisha Uchaguzi
wa mwaka huu
“Mafanikio ya uchaguzi wa mwaka huu yatatokana na ushiriki
wenu, niwasihi sana jitokezeni kwa wingi siku ya octoba 28 ili kwa pamoja
tutimize haki ya msingi nay a kikatiba ya kuchagua viongozi bora kwa hatma ya
maisha yetu na Taifa letu…’Kura yako ni Sauti yako’,” alisema John
Akizungumza na watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Singida, Makampuni
ya Mitandao ya simu (Tigo na Airtel) Hospitali ya Mkoa na Rufaa, walimu wa
shule ya Sekondari Senge na shule za msingi Sabasaba na Bomani, Afisa Utawala
huyo, alisema kila mdau akitimiza wajibu wake kwa kuzingatia sheria, kanuni,
taratibu na miongozo iliyowekwa basi watanzania wataweza kupiga kura kwa amani
siku hiyo ya uchaguzi
Kwa upande wake, Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka WOWAP,
Issah Shayo, aliwatoa hofu wapiga kura wote wenye mahitaji maalumu, akisisitiza
kuwa tayari maelekezo yametolewa kwa watendaji wote wa uchaguzi kutoa
kipaumbele vituoni kwa watu wenye ulemavu, wajawazito, wazee, wagonjwa na akinamama
wanaonyonyesha
Shayo alisema kwa wale wasiojua kusoma na kuandika ruksa
kwenda na watu wanaowaamini kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura, lakini pia
kumewekwa utaratibu madhubuti na utakaokuwa na tija kwa watu wa makundi maalumu,
katika kuhakikisha wote wenye sifa ya kupiga kura wanafanya hivyo, lengo ni
kuufanya uchaguzi wa 2020 kuwa wa kuaminika, kwa uwiano na mazingira sawa.
kwa wiki mbili mfululizo limeendelea kusambaza elimu ya
uraia ya Mpiga Kura kwa wananchi wote wa mkoa wa Singida na vitongoji vyake,
lengo likiwa ni kuhakikisha kila mwana-singida anatumia haki yake ya kikatiba
ya kuchagua viongozi sahihi kuelekea uchaguzi mkuu
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka WOWAP, Issah Shayo alisema azma hasa ya mafunzo hayo ni
kuelimisha na kuwakumbusha wananchi juu ya wajibu wao muhimu wa kuhakikisha
wanachagua viongozi bora kwa maendeleo yao katika muktadha wa kauli mbiu isemayo
‘Kura yako, Sauti yako’
“Tunawasihi wananchi wote wa Singida, ifikapo Oktoba 28
twendeni tukapige kura ili kupata viongozi watakaoamua mustakabali wa maisha
yetu na vizazi vyetu…kumbukeni kura yako ndiyo sauti yako,” alisema Shayo
Alisema shabaha ya mafunzo hayo ni kuhamasisha na kuchochea
kasi ya ongezeko la wananchi wengi zaidi kutambua haki yao ya kuchagua na
kuchaguliwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa kwa uratibu wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi
Mpaka sasa shirika hilo linaendelea kutoa mafunzo hayo
katika maeneo mbalimbali, ikiwemo kwenye majimbo ya Singida Mjini, Singida
Vijijini, Singida Kaskazini, Singida Magharibi, Manyoni Mashariki, Iramba
Mashariki na Magharibi
“Tunapita kwenye mikusanyiko na kufanya mikutano na wananchi
na kuwapatia elimu hii ya uraia, na
tunashukuru kila tunapopita mwamko ni mkubwa. Ujumbe wetu mkubwa kama
shirika la WOWAP ni kuwasihi wananchi wote wenye sifa ya kupiga kura wasipoteze
fursa hiyo muhimu ifikapo Oktoba 28,” alisema Afisa Utawala wa Shirika hilo,
Loveness John.