Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Peter Ngamilo wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya biashara ya TANTRADE viwanja vya JK Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
……………………………………………
Akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Peter Ngamilo amesema kuwa wanashauri Watu wanapotumia simu zaidi ya dakika tano kutumia ‘Earphone’ au kuweka ‘Loudspeaker’ kuepuka madhara ya mionzi huku wakieleza matumizi ya simu hizo ikiwa imeisha au inalalamika chaji ni hatari zaidi kwani mionzi inakuwa mikubwa.
Wananchi kukabiliana na mionzi iliyopo katika simu za mkononi za kisasa kwa kuzungumza chini ya dakika tano vinginevyo inaweza sababisha madhara mbalimbali mwilini.
Ametaja baadhi ya madhara yanayoweza kupatikana ni ugonjwa wa Saratani huku wakitaka kuacha kuwapatia watoto kutumia simu hizo mara kwa mara kwani mionzi yake inaathiri mifumo ya ukuaji kwa watoto.
Ngamilo amefafanua wananchi kuwa lengo la kuwapo katika maonesho hayo ni kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kukabiliana na mionzi katika shughuli zao za kila siku.
“Mionzi ya simu iko katika aina ya mionzi ambayo haileti madhara ya moja kwa moja lakini unapozungunza kwa muda mrefu inaweza kusababisha kichwa kuuma au joto la mwili kupanda huku kwa watoto wadogo ubongo bado ni teke na wako katika ukuaji hivyo kuweza kuharibu ukuaji,” amesema.
Ameongeza kuwa wanawashauri wazazi matumizi ya simu za mkononi hasa hizi Smartphone kwa watoto ,siyo mazui na kama wanatumia ni vema earphone au kuwawekea loudspeaker.
Ametumia nafasi hiyo kushauri kuwa simu ikiwa chaji ndogo isitumike kwani mionzi inakuwa katika hatua kubwa na kuchaji tena huku kwa wale wanaopenda kulala na simu kwa kuweka pembeni ya mito ni hatari kwani mionzi inakuwa kwa kasi zaidi.
Akizungumzia katika sekta ya Afyamionzi amesema ina madhara kwa wanawake wenye mimba changa, hivyo ukitakiwa kupiga X-Ray kumwalifu Daktari kwani mionzi itaathiri kiumbe kilichopo tumboni na kuzaa mtoto mwenye mapungufu.
Amesema katika vipimo vya X-Ray na CT -Scan ni vipimo haviwezi kuepuka kutokana na madaktari kutaka kufahamu ukubwa wa tatizo kwa mgonjwa ila ni vema wagonjwa kujiridhisha kama mtaalam huyo anaruhusiwa na leseni za kutoa huduma kwani unaweza kuzidisha au kupunguza dozi kwa metu mnene au mwembamba na kulazimu daktari kurudiwa.
Ametoa rai kwa wananchi kufuatilia kama vituo vinavyotoa vipimo hivyo wana leseni ,kama hawana leseni ya tume inawezekana ajakidhi taratibiu na kutoa matibabu kinyume cha taratibu .
“Tunawaomba wananchi kuwa makini katika kupata huduma za afya hususan vipimo vyenye kama vipimo vya x- Ray , CT scan, Gama Camera na vinginevyo wakati tume hiyyo ikiendelea kukagua vituo mbalimbali vya afya kuhakikisha usalama wa wananchi,” amesema Ngami.
Kuhusu mionzi inayotolewa kwa wagonjwa wa saratani, Ngami amesema inasaidia kuua seli zilizoleta madhara kwa wagonjwa pale inapokuwa mgonjwa yuko katika hatua za awali na kupona kabisa.
Pamoja na mambo mengine amewahamasisha wananchi wanaofika kwenye maonesho hayo kutembelea kwenye banda lao ili kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo yanayohusu mionzi.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akimsikiliza akitoa magizo kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Peter Ngamilo wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya biashara ya TANTRADE viwanja vya JK Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Sylvia Lupembe.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akiagana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Peter Ngamilo mara baada ya kutembelea banda hilo.