Mkurugenzi wa Biashara TTCL, Bw.Vedastus Mwita aqkizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja uliofanyika Makao Mkuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Biashara TTCL, Bw.Vedastus Mwita akiwalisha keki baadhi ya wateja katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja uliofanyika Makao Mkuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Biashara TTCL, Bw.Vedastus Mwita akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Shirika hilo katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja uliofanyika Makao Mkuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL wakiwahudumia wateja wao katika ofisi za Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
******************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesherehekea wikiya huduma kwa wateja kwa kuwaleta wateja wao karibu ambapo wanapata fursa ya kuonana nao , kupata maoni yao kuhusu huduma wanayoipata na kuwapa majibu juu ya changamoto wanazokutana nazo kwenye huduma za Shirika hilo.
Ameyasema hayo leo Mkurugenzi wa Biashara TTCL, Bw.Vedastus Mwita katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja uliofanyika Makao Mkuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo Bw.Mwita amesema pamoja na uwepo wa Wiki ya huduma kwa Wateja wataendelea kutoa huduma iliyotukuka kwa wateja wao kabla, wakati na baada ya kununua bidhaa au kupatiwa huduma husika ili kukidhi kiwango na matarajio ya mteja.
“Katika kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma kwa wakati TTCL tumeendelea kubuni njia mbalimbali ambazo wateja wetu wanaweza kuuliza, kutoa maoni na kero mbalimbali na kuweza kujibiwa na watoa huduma wetu kwa haraka zaidi”. Amesema Bw.Mwita.
Aidha, Bw.Mwita amesema njia ambazo wateja wao wanaweza kuuliza ni pamoja na kituo cha huduma kwa wateja (namba 100), website na mitandao ya kijamii ambapo mteja anaweza kueleza changamoto zake na kuhudumiwa wakati wowote.
Pamoja na hayo TTCL imewashakuru wateja wao wa ndani na wale wa nje ya nchi kama vile Uganda, Rwanda, Burundi,Zambia,Kenya na Malawi kwa kuendelea kuwaamini na kutumia huduma za TTCL za Data na Sauti (Voice).