Home Mchanganyiko DC MGEMA ATOA BAISKELI KWA WALEMAVU

DC MGEMA ATOA BAISKELI KWA WALEMAVU

0

Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akimkabidhi mkazi wa mtaa wa Bombambili katika Manispaa ya Songea Frowin Fungo ambaye ni mlemavu wa miguu fedha taslimu shilingi laki 1 ili ziweze kumsaidia kuongeza mtaji katika shughuli zake za kushona viatu ambapo pia alimpa Baiskeli ya magurudumu matatu ambayo itamwezesha kutoka nyumbani na kwenda katika shughuli zake.

Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema kushoto akimsikiliza mkazi wa kijiji cha Mpitimbi Aron Ponera anayejishughulisha na kilimo baada ya kumpa baiskeli ya magurudumu matatu itakayomwezesha kwenda na kurudi shambani,
Ponera licha ya ulemavu wake lakini amekuwa akijishughulisha na kilimo kwa ajili ya familia.

Picha zote na Muhidin Amri

************************************

 Na Muhidin Amri,
Songea

MKUU wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma  Pololet Mgema,amewataka vijana wilayani humo kuhakikisha wanajiunga katika vikundi ili iwe rahisi kwa serikali kupitia halmashauri za wilaya kuwapa mikopo  isio na riba  ambayo itawawezesha kuanzisha vikundi vya kiuchumi  na kujikwamua na umaskini.

Amesema hayo jana wakati akikabidhi msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu na fedha shilingi laki moja kwa mkazi  wa mtaa wa Bombambili manispaa ya Songea Frowin Fungo ambaye ni mlemavu wa miguu anayejishuhulisha kushona na kung’arisha viatu  katika kituo cha mabasi cha Mfaranyaki manispaa ya Songea.

Alisema, Fungo amefika ofisi ya mkuu wa wilaya mara tatu  kuomba  fedha ili aongeze  mtaji wake, kwa hiyo aliwasilina na wadau kwa ajili ya kupata baiskeli ambayo itamsaidia kwenda na kurudi katika shughuli zake za kila siku.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya, Fungo amepata msaada wa baiskeli na fedha hizo kutokana na yeye mwenyewe kuanza kuchukua hatua  na kuanzisha shughuli ambayo ina muingizia kipato kinachomsaidia kuendesha maisha yake licha ya ulemavu alionao badala ya kukaa barabarani na kuomba omba kwa wapiti njia.

Alisema, kama walemavu na vijana wakiungana pamoja itakuwa rahisi kwa halma

DC MGEMA ATOA BAISKELI KWA WALEMAVU

shauri kuwapa mikopo ambayo inarejeshwa kwa kipindi cha muda wa miaka mmoja tena bila riba yoyote.

Mbali na Fungo,pia mkuu wa wilaya amemkabidhi mkazi wa kijiji cha Mpitimbi  ambaye pia ni mlemavu wa miguu anayejishughulisha na kilimo Aron Ponera, mwenye mke na watoto watano baiskeli ili iweze kumsaidia kwenda shambani na kurudi nyumbani badala ya kutambaa kwa magoti

Alisema, suala la ulemavu halimpi haki mtu kuwa omba omba,kwa hiyo walemavu ni kama sehemu ya jamii ni lazima wawe wabunifu kwa kuanzisha miradi midogo ya kiuchumi ambayo mbali na kuwaingizia kipato pia itawaondolea aibu ya kudharauliwa  na jamii.

Alisema, watu wenye ulemavu wana uwezo wa kufanya kazi na hivyo ulemavuo sio kizuizi cha kufanya kazi kama ilivyo kwa Ponera ndiyo maana serikali na wadau wengine wakaona ni vema kumsaidia baiskeli ili iweze kumsaidia katika safari zake za kimaisha.

Pia mkuu wa wilaya amehaidi kumsaidia mbolea kwa ajili ya shughuli zake za kilimo ili aweze kuzalisha kwa wingi mazao  yatakayomsaidia  yeye na familia yake  kama chakula na  kiasi kingine kuuza ili aweze kupata fedha.

Amempongeza Ponera kwa kujituma na kuwataka walemavu  na wale wasio walemavu kuiga mfano mzuri wa Ponera ambaye kila mwaka anatumia muda mwingi katika shughuli za kilimo  badala ya kukaa nyumbani  na kusubiri msaada kutoka kwa watu wengine.

Aidha Mgema, amewataka watu wenye uwezo kuwa na  huruma kwa kuwasaidia watu wengine wenye mahitaji maalum ikiwemo walemavu ambao kutokana na upungufu wa baadhi ya viungo vya miili yao ni shida sana kuweza kupambana na maisha ya kila siku.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Ponera na Fungo wamemshukuru mkuu wa wilaya kwa huruma yake ambayo imewawezesha kupata baiskeli hizo ambazo zitawasaidia katika shughuli zao za kujitafutia ridhiki.

Fungo alisema, kwa muda mrefu shida yake kubwa ilikuwa ni kupata usafiri wa kutoka nyumbani hadi kwenda katika shughuli zake  kutokana na changamoto anazo kutana nazo kwenye usafiri wa umma kama daladala kwani baadhi ya watu walimchukulia kama kiumbe asiye na thamani.

Alisema, baiskeli hiyo imemaliza kilio chake cha muda mrefu  na kuhaidi kuitunza na kuitumia vizuri na itakuwa sehemu ya mafanikio  yake katika maisha.

Kwa upande wake Aron Msigwa,amewashukuru wadau wote wakiongozwa na mkuu wa wilaya kwa moyo wao kumsaidia baiskeli ambayo itamsaidia kumfikisha shambani na wakati mwingine kuitumia katika majukumu mengine ya kijamii.