Kamishna
Msaidizi wa
Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Grace Lobora akizungumza kuhusu
tukio la kukamatwa kwa wahamiaji haramu karibu na hifadhi ya Taifa ya
Saadani
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius
Chatanda akizungumza kuhusu tukio hilo kulia ni Mkuu wa wilaya ya
Pangani Zainabu Abdallah Issa kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Baraka Batenga
Kamishna
Msaidizi wa
Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Grace Lobora kushoto
akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina
Matagi wakati wa tukio hilo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius
Chatanda kushoto akisisitiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Pangani kulia Zainabu Abdallah Issa na anayefuatia ni Kamishna Msaidizi wa
Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Grace Lobora
Kamishna
Msaidizi wa
Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Grace Lobora kushoto akisisitiza
jambo wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda kuhusu namna
walivyofanikisha ukamataji huo wa wahamiaji haramu
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda kushoto akiwa na Mkuu wa
Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi wakiwahoji wahamiaji
haramu hao
Mkuu
wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi kulia akisisitiza
jambo wakati akieleza namna wahamiaji hao walivyokamatwa
ASKARI wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wilayani Pangani wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 32 waliokutwa wakiwa karibu na hifadhi hiyo wakisafirishwa kupelekwa nchi za kusini mwa Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa wahamiaji hao Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Grace Lobora alisema kwamba wahamiaji hao walikamatwa Septemba 27 mwaka huu usiku.
Alisema ukamatwa huo waliofanya baada ya kupata taarifa kutoka wananchi wa Kijiji cha Buyuni kupitia Mwenyekiti wa Kijiji hicho Diwani Akida ambaye aliwaeleza uwepo wa mazingira yasiyoridhisha kwenye eneo lake hasa eneo la bahari baada ya boti moja kukwama.
Alisema baada ya kupata taarifa hiyo wao kama wahifadhi wana jukumu la kulinda maliasili na kuangalia usalama kwenye miji yote inayowazunguka waliandaa kikosi kazi cha kwanza waliokwenda eneo la tukio na walipofika waliwakuta wahamiaji hao eneo la bahari karibu na hifadhi hiyo katika kijiji cha Buyuni.
“Tulipofika tuliwaweka chini ya ulinzi na baadae tukawasiliana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi ambaye alitoa ushirikiano mkubwa kwa sababu wanaandaa askari kwa kuwapa msaada baada ya kuangalia umbali kutoka Pangani mpaka eneo la tukio”Alisema
Alisema baadae hapo waliamua kutuma kikosi cha pili na ndipo walipofika na kufanikiwa kukaweka chini ya ulinzi wahamiaji 28 ambao ni raia wa Ethiopia lakini alfarji ya leo wakapata taarifa nyengine ya uwepo wa wahamiaji wengine wanne ambao ni raia wa Somalia na wakatuma kikosi na kufanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi.
“Kati yao wapo wahamiaji 32 raia wa Ethiopia 28 na raia wa Somalia wanne akiwemo mwanamke mmoja kwa hiyo baada ya kufanikisha tukio hilo tumewafikisha na kuwakabidhi kwenye mamlaka ya Polisi kwa ajili ya hatua zaidi”Alisema
Awali akizungumza kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda aliwapongeza askari wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa kazi nzuri kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Polisi wilaya ya Pangani.
“Kwa kweli niwapongeze askari wa hifadhi ya Taifa ya Saadani ka kazi nzuri kufanikisha kukamatwa kwa wahamiaji hao kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Pangani niwaambie tu kwamba mawakala wanaojishughulisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu mkoani Tanga hawatasalimika tutawasaka popote iwe ni nchi kavu,majini na kisha kufikishwa mahakamani
Hata hivyo ametangaza vita mpya kwa mawakala wanaojishuhulisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu mkoani Tanga kwamba hawatasalimika watasakwa popote iwe ni nchi kavu, majini na kisha kufikishwa mahakamani.
Alisema juhudi hizo ni nzuri na zinapaswa kuwa endelevu ili kuweza kuhakikisha wahamiaji haramu hawapiti tena kwenye maeneo hayo ikiwemo wananchi kuendelea kuwafichua wanapowaona watu na kuwatilia mashaka.
“Labda niwaambie tu kwamba wale wanaojihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu mkoani hapa hawatabaki salama kwa sababu huo ni uhalifu unaovuta mipaka na uhalifu huu hauwezi kukubalika hapa nchini”Alisema
“Sisi sote tunafahamu kinachoendelea nchini Somalia tunauhakika gani wanaweze wakawa wanapita wakaenda hawawezi kwenda kuungana na wenzao nchini msumbiji …tuna uhakika gani hawawezi kubaki masalia nchini wakafanya wanayoyafanya huko walipotoka”Alisema
Naye kwa upande wake Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Baraka Batenga alisema ni kweli lipo wimbo la wahamiji haramu kutoa pembe ya afrika kuja Tanzania kwa nia ya kupitia kwenda kusini mwa Afrika kwea lengo la kwenda kujitafutia maisha bora.
Alisema katikati kulikuwa kumetulia hasa kwenye kipidi cha ugonjwa wa Corona labda wanaamini hiyo ilitokana na majirani zao walikuwa wameweka vizuizi vya watu kutoka sehemu moja kwenda jengine.
Alisema lakini hivi karibuni wimbi hilo limeanza kupanda na wao wanakabilia nalo na walianza kukabiliana nalo kwa wilaya za Mkinga ambao wanaingilia maeneo ya moa,jasini kupitia mwakijembe kwa sasa wameweka task force ndogo kama sehemu ya mkakati ya kukabilia na wimbi la wahaamiaji haramu na wamekuwa na mafanikio makubwa na kuweza kudhibiti kwa kiasi kikubwa.
“Kwani Katika kipindi cha Agosti mpaka leo wilaya ya Mkinga wamekamatwa wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia 37 na Muheza 7, Handeni waethipia 8 ambao walikuwa hawakutani nao ni wasomali na hivyo ni kesi ya kwanza kutokana na kwamba hawajakamtwa muda mrefu”Alisema
Hata hivyo alisema wanaofanya mambo hayo ni watanzania na kibaya zaidi hivi karibuni wilaya ya Muheza walimkamata mwenyekiti wa kijiji cha Upare naye ameingia kwenye kundi hilo hawakumuacha salama yupo kwenye mikono ya sheria .
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Buyuni Diwani Akida alisema kijiji hicho kimepakana na hifadhi ya Taifa ya Saadani alisema hali ya usalama sio nzuri kiupande wao huku wanawashukuru wenzao wa hifadhi ya Taifa ya Saadani wanatoa msaada sana kwao wakati panapojitokeza matatizo yoyote wanakuwa karibu kuwasaidia.
Alisema kama Septemba 27 mwaka huu saa moja usiku walifika wasomali na boti yao hatukujua wana silaha gani lakini walipofika ikabidhi tukawazingira na kutoa taarifa kwa Saadani kwa sababu wapo wakafika wakawadhibiti na baadae pia kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wilaya ya Pangani walipofika wakawachukua.