Afisa mdhibiti ubora Sileja Lushibika akizungumza na mmoja wa Wazalishaji mafuta ya kula Mkoani Singida baada ya kutembelea Wazalishaji hao na kuwapatia elimu ya usindikaji wa mafuta.Meneja wa Mafunzo na Utafiti TBS Bw. Hamisi Mwanasala, akitoa elimu ya vifungashio kwa wadau wa mafuta ya kula yanayoendelea kanda ya kati, katika ukumbi wa shule ya sekondari Shelui wilaya ya Iramba.
********************************
Wazalishaji na wauzaji wa mafuta ya kula wametakiwa kufuata kanuni za usindikaji wa mafuta ili kuweza kuzalisha bidhaa iliyobora na kumlinda mlaji.
Akizungumza na baadhi ya wasindikaji wa Mafuta ya Kula Mkoani Singida Afisa mdhibiti ubora Sileja Lushibika amesema sio kila mtu anaruhusiwa kuingia katika eneo la usindikaji ili kuzuia bidhaa inayozalishwa kuwa na uchafuzi na anaeruhusiwa kuingia katika eneo la usindikaji ni yule ambaye amefuata kanuni zote.
Nae Meneja wa Mafunzo na Utafiti Hamisi Sudi amewataka wasindikaji hao kueleza changamoto zao mahali husika ili kuweza kutatuliwa changamoto ambazo zinawakabili na baadae kukuza biashara zao na kufikia malengo yao.
“Kama mkiwa na changamoto zenu, maafisa biashara wapo,maafisa SIDO wapo ombeni nafasi ya kupata elimu hii wale wakisikia kilio chenu watawaita taasisi inayohusika na kuwasaidia”.
Hata hivyo kwa upande wake Meneja wa Mafunzo na Utafiti TBS Bw. Hamisi Mwanasala, akitoa elimu ya vifungashio kwa wadau wa mafuta ya kula yanayoendelea kanda ya kati, katika ukumbi wa shule ya sekondari Shelui wilaya ya Iramba amesema ili vifungashio viwe bora vinatakiwa kuwa na vitu mbalimbali ikiwemo jina la biashara (Bidhaa inayowekwa kwenye kifungashio),anuani ya mzalishaji, uzito na ujazo,namba ya toleo,utunzaji,taarifa za kutumia/kuuza.