Na. Salama Namga-MAELEZO.
Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman ameagwa rasmi kimahakama baada ya kustaafu utumishi wa umma, baada ya kuhudumu katika Muhimili huo kama Jaji Mkuu kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi mwaka 2017, katika sherehe ya kumuaga iliyofanyika leo katika Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam.
Jaji Othman Chande ameushukuru uongozi wa Serikali kuanzia Awamu ya Tatu chini ya Benjamin William Mkapa kwa kumpa dhamana ya kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, pamoja na Rais wa Awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, na hatimaye Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kumuamini na kufanya nao kazi hadi alipostaafu mwaka 2017.
Jaji Chande amesema Mahakama ya Tanzania inazingatia mgawanyo wa madaraka katika utendaji kazi wake, na kuyafanyia kazi maoni ya umma pale yanapokusanywa ili kuweza kuboresha na kuimarisha huduma za kimahakama ili hatimaye ziweze kuwafikia wananchi kwa wakati.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma amemueleza Jaji Othman kuwa, Serikali inatambua umuhimu wake na kazi zake alizofanya zimekuwa chachu ya maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika katika Mahakama ya Tanzania.
“Serikali inatambua umuhimu na mchango wako katika kuimarisha maboresho ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi katika Mahaka ya Tanzania, pia tutaendelea kuufanyia kazi ushauri wako ambao unaendelea kutupatia kama Jaji mkuu mstaafu”Alisema Prof. Juma.
Nao baadhi ya Majaji waliohudhuria katika hafla hiyo, wamemwelezea Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande kuwa ni mtu mwenye weledi na anayesimamia Sheria za Mahakama, na ametoa mchango mkubwa katika maboresho yanayoendelea katika Mahakama na wataendelea kumuenzi kwa vitendo kwa kutumia busara zake na hekima aliyonayo katika kazi zao za kila siku.
Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman alizaliwa tarehe 1 Januari, 1952, ana Shahada ya kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na Shahada ya Uzamili (MA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Webster cha huko Geneve Uswisi.
Amewahi kuwa Makamu wa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya mauaji ya Rwanda (ICTR) huko Jijini Arusha na amewahi kushika nafasi sawa na ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko TimoriMashariki.
Kadhalika Jaji Othman, amewahi kufanya kazi ndani na nje ya nchi katika Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kama vile Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Msalaba Mwekundu. Pia ni mtaalam mbobezi katika masuala masuala ya Sheria za haki za binadamu.
Na. Salama Namga-MAELEZO.Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman ameagwa rasmi kimahakama baada ya kustaafu utumishi wa umma, baada ya kuhudumu katika Muhimili huo kama Jaji Mkuu kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi mwaka 2017, katika sherehe ya kumuaga iliyofanyika leo katika Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam.Jaji Othman Chande ameushukuru uongozi wa Serikali kuanzia Awamu ya Tatu chini ya Benjamin William Mkapa kwa kumpa dhamana ya kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, pamoja na Rais wa Awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, na hatimaye Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kumuamini na kufanya nao kazi hadi alipostaafu mwaka 2017.Jaji Chande amesema Mahakama ya Tanzania inazingatia mgawanyo wa madaraka katika utendaji kazi wake, na kuyafanyia kazi maoni ya umma pale yanapokusanywa ili kuweza kuboresha na kuimarisha huduma za kimahakama ili hatimaye ziweze kuwafikia wananchi kwa wakati.Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma amemueleza Jaji Othman kuwa, Serikali inatambua umuhimu wake na kazi zake alizofanya zimekuwa chachu ya maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika katika Mahakama ya Tanzania.“Serikali inatambua umuhimu na mchango wako katika kuimarisha maboresho ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi katika Mahaka ya Tanzania, pia tutaendelea kuufanyia kazi ushauri wako ambao unaendelea kutupatia kama Jaji mkuu mstaafu”Alisema Prof. Juma.Nao baadhi ya Majaji waliohudhuria katika hafla hiyo, wamemwelezea Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande kuwa ni mtu mwenye weledi na anayesimamia Sheria za Mahakama, na ametoa mchango mkubwa katika maboresho yanayoendelea katika Mahakama na wataendelea kumuenzi kwa vitendo kwa kutumia busara zake na hekima aliyonayo katika kazi zao za kila siku.Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman alizaliwa tarehe 1 Januari, 1952, ana Shahada ya kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na Shahada ya Uzamili (MA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Webster cha huko Geneve Uswisi.Amewahi kuwa Makamu wa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya mauaji ya Rwanda (ICTR) huko Jijini Arusha na amewahi kushika nafasi sawa na ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko TimoriMashariki.Kadhalika Jaji Othman, amewahi kufanya kazi ndani na nje ya nchi katika Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kama vile Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Msalaba Mwekundu. Pia ni mtaalam mbobezi katika masuala masuala ya Sheria za haki za binadamu.