Waziri wa Afya, Mhe Ummy Mwalimu akihutubia Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa waliofika katika Mkutano unaoanza leo jijini Dodoma
………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu ametaja maeneo matatu muhimu katika mpango wa muda mfupi na mrefu katika hospitali za rufaa za mkoa kwa lengo la kutofautisha hospitali hizo na vituo vya afya.
Waziri ummy ameyasema hayo jijini hapa leo wakati akifungua mkutano wa viongozi wa hospitali za rufaa za mkoa ambapo amesema maeneo hayo matuta yakipatiwa ufumbuzi yatasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo.
Eneo la kwanza amesema ni kila hospitali ya rufaa za Mikoa kuwa na madaktari bingwa katika huduma za kibingwa 13 akitole mfano huduma ya moyo, Kunywa, masikio, meno pamoja na huduma ya mama na mtoto.
Eneo lingine amesema ni miundombinu hususani katika huduma za ICU, pamoja na huduma za zarura na ajali.
Eneo la tatu ni mama na mtoto hususani huduma ya ICU ya mama pamoja na ya mtoto.
Hata hivyo amewataka viongozi hao kupitia kikao chao kuangali maeneo mengine ambayo yanaweza kutekelezwa katika mpango huo wa muda mfupi na mrefu.
Amesema kupitia utekelezaji huo hospitali hizo zitakuwa mfano kwa vituo vya afya vya kutoleoa huduma za afya.
Kwa upande wake naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dk Faustine Ndungulile amesema bado wanapokea malalamiko kutoka kwa wananchi pamoja na baadhi ya watumishi wa taasisi.
Amesema kazi ya waganga wafawidhi sio kukaa ofisini bali ni kusikiliza na kutumia changamoto mbalimbali akisema ni lazima kuwa na mfumo mzuri wa kutatua malamiko hayo.
Hata hivyo alikumbushia agizo la kila mtumishi wa afya kuwa na kitambulisho ili kuwabaini wale wote wanaofanya azidi bila kuzingatia miiko ya kazi.
Alisema hiyo itasaidia kukaa nani kafanya nini na kwa wakati Gabi.
Kuhusu suala la mapato alisema hospitali za rufaa za mkoani zitashindanishwa katika ukusanyaji wa mapato akisema fedha hizo zinasaidia kuimarisha huduma za afya.