Home Mchanganyiko RUWASA YAANZA KUFANYA KAZI RASMI

RUWASA YAANZA KUFANYA KAZI RASMI

0

Na EZEKIEL NASHON, DODOMA.

KATIBU mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitilya Mkumbo, ametangaza rasmi kuanza kufanya kazi rasmi  kwa Wakala wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingiria (Ruwasa) Julai mosi mwaka huu, huku wananchi wa vijijini wanaofikiwa na huduma ya maji ikifikia asilimia 64.8.

Profesa Mkumbo, ametangaza hayo leo Jijini  Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanza kufanya kazi kwa wakala huo na kuhusu mkutano wa Saba wa mwaka wa Bodi za maji za mabonde utakaofanyika kuanzia Julai 9 hadi 11 mwaka huu mkoani Kigoma Ujiji.

Amesema mamlaka hiyo imeanza kufanya kazi rasmi leo july,  mosi na itazinduliwa rasmi july 16 mwaka huu, lakini  kuanzia leo itaendelea kufanya kazi kama kawaida, utasaidia sana utapikanaji wa maji safi na salama kwa maeneo ya vijijini.

Amebainisha kuwa mpaka kufikia Aprili mwaka huu jumla ya vituo vya kuchotea maji vilikuwa 131370 vilikuwa vimejengwa vijijini na vilipaswa kuhudumia watu milioni 32.8 sawa na na asilimia 83 lakini ni vituo 86,700 sawa na asilimia 65.6 pekee ndivyo vinavyofanya kazi vikihudumia watu milioni 25.3 sawa asilimia 64.8 ya wananchi washio vijijini.

Profesa Mkumbo amefafanua kuwa hiyo ni changamoto kubwa na kwamba sekta ya maji vijijini inakabiliwa na usimamizi hafifu wa maji pamoja nab zingine hali hiyo inasababishwa na wahandisi maji kuwajibika kwa mamlaka zaidi ya moja na hivyo kutumika kwa zaidi ya kazi ya ujenzi wa miradi ya maji.

“Ili kukabiliana na changamoto za kimfumo zinazokabili sekta ya maji nchini Rais Dk John Magufuli Mei 10 mwaka jana alitoa maelekezo ya kisera kuwa watumishi wote wa sekta ya maji wahamishiwe Wizara ya Maji ndio  tukaamua kuunda mamlaka hii,”amesema.

Amewataja maofisa walioteuliwa kukaimu nafasi mbalimbali za uongozi wa RUWASA katika ngazi ya kitaifa na mikoa wameshateuliwa nao ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Gonsalves Rutakyamirwa, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji maji na usafi wa Mazingira, Mkama Bwire.

Alibainisha kuwa wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi, Deusidet Magoma, Kaimu Mkurungezi wa Mipango na Uratibu wa CBWSOs Enock Wagala, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Sheria, Gloria Chegeni, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ndani Herieth Kaiza.

Wengine walioteuliwa ni maofisa watakaokaimu nafasi ya Meneja wa RUWASA katika mikoa na mikoa waliyopangiwa, ni Joseph Makaidi mkoa wa Arusha, Godfrey Kabula mkoa wa Dodoma, Nicas Ligombi mkoa wa Geita, Shaban Jellan mkoa wa Iringa, Sylivester Paulini mkoa wa Katavi, Mathius Mwenda Mkoa wa Kigoma, Frank Elisa mkoa wa Kilimanjaro, Renatus Gumba mkoa wa Lindi.

Kwa upande wa mkoa wa Manyara aliyeteuliwa ni Mary Mbowe, mkoa wa Mara Muhibu Lubasa, mkoa wa Mbeya Mathayo Athmani, mkoa wa Morogoro Emmanuel Alexandar, mkoa wa Mtwara, Mbaraka Ally, mkoa wa Mwanza Warioba Sanya na Frederick Magige mkoa wa Njombe.

Wengine kuwa, mkoa wa Pwani Beatrice Kasimbazi, mkoa wa Rukwa Shaaban Daud, mkoa wa Ruvuma Hans Nestory, mkoa wa Shinyanga Julieth Mganga, mkoa wa Simiyu Hatari Kapufi, mkoa wa Singida Genes Kimaro, mkoa wa Songwe Pambe Pambe, mkoa wa Tanga John Msengi na Mariam Majala mkoa wa Tabora.

Profesa. Kitila alisema tayari wameshateua majina katika mikoa 24 na kwamba umebaki mkoa mmoja wa Kagera bado hawajateua na atateuliwa baadaye.

Aidha ametumia nafasi hiyo kutangaza  mkutano mkuu wa Saba wa Bodi za Maji za Mabonde, kuwa utafanyika katika mkoa wa Kigoma  Ujiji, utakao kuwa na kauli mbiu ni Rasilimali za Maji ni Msingi wa Maendeleo Endelevu ambayo inalenga kuonesha uhusiano mkubwa uliopo kati ya uwepo wa rasilimali za maji na maendeleo ya nchi pamoja na ustawi wa jamii.

“Katika mkutano huo utakaofanyikia ukumbi wa NSSF Manispaa ya Kigoma Ujiji, mgeni rasmi atakuwa waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, mwenyeji wa mkutano huo atakuwa Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Tanganyika ambayo makao yake makuu ni Kigoma,amesema  prof Mkumbo.

Pamoja na umuhimu na kazi kubwa ya kusambaza maji, kazi hiyo ni ya muda mfupi na itafikia wakati itakamilika lakini changamoto za maji ili kujihusishia usalama wa maji kwa ajili ya matumizi mtambuka.