Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya Wananchi wa mkoa wa Kagera katika mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 16 Septemba, 2020.
Sehemu ya Wananchi wa mkoa wa Kagera waliokusanyika katika Viwanja vya Gymkhana kumsikiliza Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Septemba, 202.
……………………………………
NA JOHN BUKUKU-BUKOBA- KAGERA
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amesema tani zipatazo 24 .62 za bati au Tin zimeuzwa kwenye soko la Tin Kyerwa,na dhahabu imeongezeka uzalishaji ambapo mgodi Stamigo uliopo Bihalamulo unazalisha kilo 2069.31 zenye thamani ya dola za marekani Milioni 69 .57,”.
Kuanzishwa kwa soko la dhahabu hapa, ndiyo hatua zilizoachangia sekta ya madini kuipiku sekta ya utalii katika kuingizia fedha nyingi za kigeni serikali.
Rais Dk.Magufuli ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Gymkana mjini Bukoba wakati akizugumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza ili kumsikiliza.
Ameongeza kuwa hayo yote yameelezwa vizuri katika ilani ya yauchaguzi ya CCM ya 2025 katika ukurasa wa 111 hadi 112.
“Tumejipanga kuimarisha udhibiti na usimamizi wa wachimbaji wakubwa na kuimarisha masoko na kuongeza maeneo ya wachimbaji wadogo wadogo katika kuwapatia mafunzo na vifaa” Amesema Rais Dk. Magufuli.
Akizungumzia Miundombinu amesema wanabukoba wanafahamu na nimashahidi kutokana na kuzama kwa meli ya Mv Bukoba ambapo tulipoteza wapendwa wetu wengi na baada ya kuharibika kwa meli ya Mv Victoria na Mv.Butihama huduma ya usafiri ilisimama kwa miaka 10 hii ilisababisha usumbufu kwa wananchi wakiwemo wafanyabiashara,”amesema
Dkt.Magufuli amesema kama alivyohaidi kwenye miaka mitano iliyopita amefanikiwa kufufua usafiri katika ziwa Victoria ,ambapo meli ya Mv Victoria “Hapa kazi tu” Maarufu kwa jina la Mama Koku imeanza kufanya kazi.
Kufufuliwa kwa meli hii na kujenga meli mpya kutawafanya wafanyabiashara waliokuwa wakipata shida na kulazimika kuzunguka umbali mrefu na kulipia gharama kubwa za usafiri sasa watasafirisha mizigo yao kwa gharama nafuu zaidi ya ilivyokuwa wakati hakuna meli.
Wakati meli ya Mv Victoria haifanyi kazi kusafirisha mizigo Bukoba tani moja ya ndizi au maharage ilikuwa inalipiwa 120,000 hadi 130,000 sasa baada ya kutengenezwa kwa meli hii wanalipa 27000.
“Hivi sasa tumeanza kutengeneza meli kubwa kwa gharama ya bilioni 90,na hii meli itakuwa kubwa zaidi itakuwa inabeba watu zaidi ya 1200 na tani za mizigo 400, Hii itasaidia sana kupunguza usumbufu kwa wananchi wa Bukoba na maeneo mengine ya kanda ya ziwa wanaotumia usafiri wa meli katika ziwa Victoria
Amesema waasisi wa taifa la Uganda ,Kenya na Tanzania walikuwa wanaunganisha usafiri wa ziwa Victoria na sisi tunataka urudi kama ulivyokuwa zamani.
“Mtu akitoka hapa katika bandari ya Bukoba aende Kemondo mahali alipokuwa anafanya biashara ya ndizi Katibu wangu Mkuu wa CCM .Dkt.Bashiru Ally watu wabebe ndizi iondoke hiyo meli iende mwanza ikitoka huko iende Musoma kisha kisumu..iende Uganda ikitoka Uganda irudi Bukoba ili mzunguko wa fedha uwe mkubwa kwa wafanyabiashara watu wengi watengeneze maisha yao,”amesema
Rais Dk.Magufuli amesema hata meli zingine zitakazokuja baadaye bei itakuwa hiyo,tani moja kwa 27000 badala ya laki na 130.000 ,hapa tutakuwa tumemuwezesha mfanyabiashara kupata faida kabla ya kusafirisha mzigo wake hiyo ndio Tanzania tunayotaka na mwelekeo wa serikali ninayoiongoza na ndio mwelekeo wa ilani ya uchaguzi,”amesema na kuongeza.
Akizungumzia sekta ya utalii amesema lazima uwe na viwanja vya ndege ndio maana uwanja wa ndege wa Bukoba ulikarabatiwa na Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.
Amesema uwanja huo umeimarishwa na gharama za usafiri wa anga zilikuwa kubwa hadi kufikia milioni 1.5,ila baada ya kukarabati uwanja kwa sasa imekuwa ni chini ya Milioni moja.
Aidha amesema usafiri wa barabara umeimarishwa kwa shilingi bilioni 149.3 kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja,
Katika kuimarishaji wa amani na usalama mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa ya mipakani,iliyokuwa na changamoto nyingi hasa katika masuala ya ujambazi kipindi cha nyuma.
Ameeleza kuwa miaka ya nyuma ilikuwa ni jambo gumu na lisilowezekana kwa watu kusafiri nyakati za usiku katika mkoa wa kagera kutokana na matukio ya kihalifu.
Ndiyo maana ili kuongeza mapato fursa za kigeni na ajira kwa wananchi wetu tumetengeneza hifadhi za Burigi Chato, Ibanda, Rumanyika ili kuondoa mapori na kuimarisha usalama wa watu na mali zao.