Na Magreth Mbinga
Mwenyekiti wa umoja wa vijana Taifa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ndugu Kheri James amemuombea kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya chama hiki Mh Abasi Tarimba leo katika viwanja vya Biafra Kinondoni akiwa kama mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni kwenye Jimbo hilo.
Akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi amesema kamati kuu ya chama hiko inaendelea kusisitiza kulinda amani ya Taifa la Tanzania,umoja na mshikamano ili waweze kupata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Octoba 28 mwaka huu.
“Tunamleta kwenu mgombea Urais Dk John Magufuli ambae ameipa heshima Nchi yetu katika Nchi zingine za nje na ndani ya Afrika imani yangu mutamchagua kwa kumpatia kura za kishindo “amesema Ndg Kheri.
Pia Kheri amesema chama cha mapinduzi kitashinda kwasababu ni chama imara,kina wagombea wenye weledi ,sifa kuwapendeza Watanzania hata sera mbadala za kuendeleza nchi na kinaamini Mungu yupo hakikurupuki.
“Abasi Tarimba amekuwa miongoni mwa watu walioleta maendeleo,kuboresha michezo,anaeishi na watu wa dini zote ,halizote matajira kwa masikini na mwenye mapenzi kwa binadamu wenzake”amesema Kheri.
Aidha mgombea Ubunge huyo Ndg Abasi Tarimba amezungumza kwaajili ya kuomba kura kwa wananchi wa Jimbo hilo la Kinondoni na kusema Chama cha Mapinduzi kimemsimamisha mbele yao ili kuomba ridhaa na wampatie kura aweze kumsaidia Dk John Magufuli kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika Jimbo hilo la Kinondoni.
“Nitahakikisha katika miaka mitano ijayo itakuwa ya neema zaidi katika Jimbo hili na changamoto za Kinondoni zinaenda kuisha sababu wakazi wengi wanaishi maisha yasiyo pia wanakumbwa na janga la mafuriko mara kwa mara pindi mvua zinaponyesha nitaenda kukomesha hadha hiyo ambayo inawatesa sana wana Kinondoni”amesema Tarimba.
Vilevile Mgombea Ubunge katika Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima amemuombea kura Ndg Abasi Tarimba kwa Wanakinondoni na kusema wampatie kura pacha wake ili awezekuibadilisha Kinondoni na maisha ya wananchi wake wamchague Tarimba kwa maendeleo ya kasi.
Sanjari na hayo Mbunge aliemaliza mida wake Ndg Said Mtulya amewataka Wanakinondoni kuchagua chama cha Mapinduzi kwani viongozi wake wanafanya kazi usiki na mchana kwenye shida na raha kwaajili ya kuwaletea wananchi maendeleo.
“Chagueni Mbunge na madiwani wa chama cha mapindizi hao wa upinzani kazi yao kupinga maendeleo nilipokuwa upinzani tulikuwa tunakutana Wabunge wote wa upinzani kujadili kutoka bungeni na kumzomea Rais”amesema Mtulya.
Hatahivyo Mtulya amewaambia wana Kinondoni kuwa Rais John Magufuli alikataa kuweka karantini kwa wananchi wanyonge wakati wa ugonjwa wa Corona akaruhusu wananchi waendelee kufanya shughuli zao ambazo zinawaingizia kipato kwa yote aliyoyafanya wampe kura za kutosha.