Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Twaha Kasim armaarufu Twaha Kiduku akipokea Mkataba wake kutoka kwa mratibu Selemani Semunyu, Kiduku anatarajiwa kushuka Ulingoni dhidi ya Mkongo guy Tshibamanga Tshitundu mpambano utakaochezwa desemba 26 mwaka 2020 Next Door Arena Masaki .
Mabondia wa ngumi za kulipwa nchini Mfaume Mfaume,Dulla Mbabe, Tony Rashid, Selemani Kidunda na Ismail Galiatano katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini Mikataba yao wanayotarajia kushuka Ulingoni dhidi ya Mabondia kutoka malawi na Zimbabwe mpambano wa usiku wa Mabingwa utakaochezwa Desemba 26 mwaka 2020 Next Door Arena Masaki.
Mabondia wa ngumi za kulipwa nchini Mfaume Mfaume,Dulla Mbabe, Tony Rashid, Selemani Kidunda na Ismail Galiatano wakati wakisaini Mikataba wyao wanayotarajia kushuka Ulingoni dhidi ya Mabondia kutoka malawi na Zimbabwe mpambano utakaochezwa Desemba 26 mwaka 2020 Next Door Arena Masaki .
****************************************
BONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA KUTOKA MKOANI MOROGORO TWAHA KASIM MAARUFU (TWAHA KIDUKU) AMEUNGNA NA MABONDIA WENZAKE KUSAINI MKATABA KWAAJILI YA KUSHIRIKI PAMBANO LA USIKU WA MABINGWA LITAKALOPIGWA DECEMBA 26 MWAKA HUU.
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI WAKATI AKISAINI MKATABA KATIKA VIWANJA VYA LUGALO, KIDUKU AMESEMA AMEJIANDAA KWAAJILI YA PAMBANO HILO KWANI WAKATI WOTE AMEKUWA AKIFANYA MAZOEZI ILI KUIPEPERUSHA BENDERA PAMOJA NA KUONYESHA UWEZO WAKE ULINGONI.
KATIKA PAMBANO HILO LILILOPEWA JINA LA (USIKU WA MABINGWA) BONDIA HUYO KUTOKA MOROGORO AMESAINI MKATABA KUPIGANA NA BONDIA KUTOKA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO GUY TSHIMANGA TSHITUNDU AMBAYE WATAONYESHANA UBABE KATIKA PAMBANO HILO LA KUWANIA UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI.
AIDHA KATIKA PAMBANO HILO BONDIA TWAHA KIDUKU AMESEMA MPINZANI WAKE HUYO ATAKUA NI WA TATU KUTOKA NCHINI KONGO KATIKA HISTORIA YAKE YA MASUMBWI.
‘’KIUKWELI NISHACHEZA NA MABONDIA WA KONGO WATATU, NA HUYU NIKICHEZA NAYE ATAKUA NI BONDIA WA TATU KWASABABU NISHACHEZA NA MMOJA KULE NCHINI ZAMBIA NA KATIKA REKODI YANGU YA NGUMI, BONDIA NILIYEWAHI KUMPIGA KO MBAYA NI HUYO NILIYEPIGANA NAYE ZAMBIA ALIEKUA ANAITWA MBIYA KANGU NILIMPIGA MPAKA AKAZIMIA PALE PALE NA WA PILI NILIFANIKIWA KUCHEZA NAYE TANZANIA SIKUMALIZA ILA NILICHEZA NAYE SANA KWAHIYO ZAIDI YA YOTE NAPENDA KUWAHAKIKISHIA WATANZANIA KUWA SITAWAANGUSHA’’
MIONGONI MWA MABONDIA WALIOSAINI KUSHIRIKI PAMBANO HILO LA UBINGWA NI MFAUME MFAUME ATACHEZA NA CHIKONDIO MAKAWA, DULLA MBABE NA ALLI KIMWENDA, SELEMANI KIDUNDA ATAKAYECHEZA NA LIMBANI MASAMBA WOTE KUTOKA MALAWI NA THONY RASHID, ATAKAYECHEZA NA TINASHE MADZIWANA WA ZIMBABWE NA ISMAIL GALIATANO DHIDI YA BAINA MAZOLA.
BONDIA TWAHA KIDUKU AMEZIDI KUITENGENEZA REKODI YAKE YA MASUMBWI BAADA YA KUMSHINDA DULLAH MBABE KATIKA PAMBANO LAO LILILOFANYIKA SEPTEMER 28 MWAKA HUU KATIKA UWANJA WA UHURU DAR ES SALAAM.
KWA UPANDE WAKE BONDIA KUTOKA JWTZ SULEIMAN KIDUNDA AMEAHIDI KUFANYA VIZURI NA KULIWAKILISHA VYEMA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA NA KUIWEKA REKODI NZURI YA MASUMBWI KATIKA SIKU HIYO.