Afisa Muendeshaji wa Kampuni ya Property International Bw.George Obado akizungumza na Fullshangweblog katika maonesho ya Kimataifa ya biashara ya Tantrade viwanja vya Sabasaba leo kuhusu mkakati wa kampuni hiyo katika masuala ya uwekezeji wa Makazi na viwanda.PICHA NA JOHN BUKUKU-(FULLSHANGWEBLOG)
Afisa Muendeshaji wa Kampuni ya Property International Bw.George Obado akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea katika banda la kampuni hiyo leo katika maonesho ya Sabasaba.
Baagdhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwaonesha viwanja wananchi waliotembelea na kujionea ramani zenye ,aeneo mbalimbali yaliopimwa viwanja kwa vya kuuza kwa makazi na viwanda.
Afisa Muendeshaji wa Kampuni ya Property International Bw.George Obado akizungumza na wateja waliofika bandani hapo leo.
…………………………………………………………..
NA EMMANUEL MBATILO
Kuelekea Katika uchumi wa kati wa viwanda,Kampuni ya Property International Bw.George Obado ambayo inajihusisha na masuala ya kuuza na kukopesha Viwanja, Nyumba pamoja na Viwanda, wameanzisha mradi ambao utasaidia wananchi kujengewa nyumba kwa mkopo na marejesho yake yatafikia mpaka miaka 15.
Ameyasema hayo Afisa Muendeshaji wa Kampuni ya Property International katika maadhimisho ya Maonyesho ya biashara ynayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungmuza katika maonyesho hayo Bw. Obado amesema kuwa wameanza ujenzi wa nyumba katika maeneo mbalimbali ili kuweza kumfanya mtu aweze kukopeshwa kwa njia ya mkopo kwani kuna watu ambao wanashirikiana nao ili kuweza kumuwezesha mwananchi kupata nyumba nzuri na nafuu.
“Unaweza ukajengewa nyumba ya bedroom mbili au tatu tayari tunazo nyumba za mfano, moja ina bedroom mbili na nyingine ina bedroom tatu, wakati bei ya nyumba ya Bedroom mbili ni shilingi milioni 90 na kwa upande wa Bedroom tatu bei yake ni Shilingi Milioni 120”. Amesema Bw. Obado.
Aidha, Bw. Obado ameishukuru serikali kwa mchango ambao wameutoa kwao hasa katika utafutaji wa haraka wa hatimiliki kwani ilikuwa ni njia nyepesi na yauhakika kwao.