Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nzega mkoani Tabora katika Kampeni za Urais za CCM wakati katika Uwanja wa Parking mjini Nzega leo Jumatano Septemba 2, 2020
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-NZEGA)
Maelfu ya wananchi wakipunga mikono yao wakati Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
………………………………………………..
Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt.John Pombe Magufuli amewaomba Watanzania wkumchagua yeye kwani ahadi anazotoa ni za kweli hivyo akichaguliwa kuongoza miaka mitano mingine iliyobaki atatimiza ahadi ambazo ameahidi na kuipaisha Tanzania kama Ulaya.
Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Parking mjini Nzega mkoani Tabora, Rais Dk. Magufuli amesema ndiyo maana toka alipochaguliwa miaka mitano iliyopita hajawahi kwenda Ulaya yeye anahangaika na shida za watanzania tu.
“Toka nilipochaguliwa Sijawahi kwenda Ulaya nataka kuitengeneza Tanzania iwe ulaya ili watu wa ulaya na kwingine waje Tanzania” amesema Dk. Magufuli.
“Nawahakikishia mimi sitoi ahadi za uongo msema kweli ni mpenzi wa Mungu, sitaki nipate dhambi kwa kuwaambia uongo, napenda siku moja nifike mbinguni ili Malaika waniambie ulifanya vizuri tunakupa hata Uwaziri wa Malaika”- Amesema Dkt.Magufuli.
Aidha Magufuli amesema wapo Watu wengi wenye maneno matamu na watawaahidi kila kitu, lakini wengi ni waongo hivyo Msidanganyike na hao.
“Wapo Watu wengi wenye maneno matamu na watawaahidi kila kitu, mnafahamu Wanaume tukiwa tunatafuta Wanawake huwa tunadanganya sana, mwishowe unamuacha kijana mliyehangaika nae kisa umepata wa mjini,huko Mjini unakuta analala kwenye ngozi unaanza kujuta”.Amesema Dkt.Magufuli.
Pamoja na hayo Dkt.Magufuli amesema hashangazwi na maneno machafu ambayo anasemwa na kutukanwa yeye kwake anajari kazi tu na kuwatumikia Watanzania.
“Matusi ninayotukanwa mimi nayafurahia kwasababu hiyo ni sadaka kwa Watanzania ambao ni waajiri wangu ninaowatumikia, bora mimi matusi niyapate lakini nyinyi mpate maendeleo ya kweli, najua wanaotukana hawapendi mambo makubwa ninayofanya”. Amesema Dkt.Magufuli.
Hata hivyo Dkt.Maguguli amesema suala la maji katika wilaya ya Nzega alilikamilisha kwa kuleta maji kutoka ziwa Victoria hivyo atashangazwa kama wananchi wa Wilaya hiyo wasipomchagua.
“Maji ni muhimu,maji ni uhai, ukitaka kula maji muhimu, ukitaka kufua maji muhimu, ukitaka Mke wako akupende maji ni muhimu,ukitaka Mumeo akupende maji muhimu, leo maji tumeyafikisha Tabora kwa 95%, nitashangaa Wananchi wa Nzega mkininyima kura”.
Nipeni tena miaka mitano muone maajabu nitakayoyafanya, maendeleo hayana Chama ndio maana siku zote huwa naomba kura kwa Vyama vyote, CHADEMA nawaomba kura, ACT naomba kura, CUF na Vyama vingine hata ambao hawana Vyama wote nawaomba kura”. Amesisitiza Dkt.Magufuli.