KATIBU wa Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akitangaza majina ya wagombea wa uwakilishi walioteuliwa na Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM leo.
KATIBU wa Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akitangaza majina ya wagombea wa uwakilishi walioteuliwa na Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM leo.
……………………………………
John Bukuku Dodoma
Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole ametangaza uteuzi wa wagombea nafasi za uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi kutoka majimbo 50 ya uchaguzi.
Polepole amesema wamezingatia kupata watu imara wenye uwezo wa kujenga hoja na kukitetea chama ndani ya baraza. Hivyo, majina yaliyopita ni wale watu wanaojitambua.
“Wawakilishi ni watu wazito, ndio wanaokwenda kuamua hatma ya Wanzanzibari kwa kutunga na kupitisha sheria zinazoongoza visiwa vile, ndio watakaoangalia namna ya kuzikabili changamoto na kuzigeuza kuwa fursa kwa Wazanzibari,ndio maana tumeteua watu makini wenye weledi wa kutosha.
Haya ni baadhi ya majina ya wagombea hao pamoja na majimbo waliyotoka kwa kuzingatia mikoa na wilaya za visiwa vya Unguja na Pemba kama ifuatavyo;
Mkoa wa Kaskazini Pemba waliopitishwa na chama ni; Jimbo la Konde – Zawadi Amour Nassor, Jimbo la Micheweni – Shahidi Hamis, jimbo la Tumbe – Said Salim,jimbo la Gando- Mariam Juma.
Ameonya baadhi ya wanasiasa wanaofuatilia mambo yao badala ya kufanya kile wanachotakiwa kukiwasilisha kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CCM jengo la White House jijini Dodoma leo, Polepole amesema anashangaa kuona wanasiasa wenye umri mkuba wanakua na hoja zakubumba badala ya kuzungumza mambo ya msingi ikiwemo kuwaahidi wananchi mambo watakayoyatekeleza ikiwa watapewa ridhaa.
“Mzee yule aache kutajataja majina ya watu, tena kama mnavyoona nipo na wajumbe wa halmashauri kuu maana yake huu ni msimamo wa chama chetu, atuache. Wasitengeneze hoja za kubumba, kwa sababu anasema uongo wa wazi ili kupata umaarufu wa kisiasa, vijana wanasema ‘kiki’,” amesema Polepole.
Amebainisha kuwa muda wote ambao wanasiasa hao walishika nafasi za juu za uongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hawakuwahi hata kujenga mnara wa mita moja katika eneo alilotoka Mtambwe Pemba.
Lakini Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi imejenga miundombinu mingi ikiwemo shule na chuo cha ufundi.
“Wanzanzibari wanaita chuo cha Amali, tumejenga chuo kikubwa cha Amali pamoja na shule za bweni kule wanaita Dahalia. Vijana wanajifunza ufundi na mafunzo ya kazi mbalimbali za mikono. Ndiyo maana tunasema katika kampeni za mwaka huu tumeamua kujenga hoja badala ya kuzungumza matusi na lugha zisizo na staha au kusema sema watu,” alisema Polepole.