
Na Emmanuel J. Shilatu
Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuzindua kwa kishindo kampeni za CCM katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Jumamosi Agosti 29, 2020 kwa mafanikio makubwa na ya kuigwa.
Dkt. Magufuli ambaye ndiye anaongoza jahazi la kuinadi ilani ya CCM 2020 – 2025 ya kuombea kura ameonyesha mwanzo mzuri kwa kupata wahudhuliaji wa kutosha. Mtaji wa uhai wa chama cha kisiasa ni Watu, CCM wanao na watashinda kwa kishindo.
Wakati wale wakipauka, wakipukutika, kuisha na hakuna tena mafuriko, Dodoma leo tumeshuhudia Kujaa uwanja ambalo ni ishara ya imariko, kubaliko na ushindi kwa CCM.
Dkt. Magufuli ameonyesha CCM ni tofauti sana na wengineo ambao wameanza kampeni kwa madai lakini CCM imeanza kwa kuzindua ilani ya uchaguzi 2020 – 2025 ambao kimsingi ni mkataba wa kisera kimaendeleo kati ya chama cha kisiasa na Wananchi.
Dkt. Magufuli ameiongoza CCM kuwaeleza Watanzania amefanya nini kimaendeleo kwa ilani iliyopita na atafanya nini akipewa tena ridhaa.
Wakati wengineo wanaohubiri uhuru wa vyombo vya habari ndio hao hao wanaofukuza vyombo vya habari kwenye mikutano yao. Lakini Dkt. Magufuli hatujamsikia akitimua vyombo vya habari. Hakika CCM ndio chama pekee nchini kinachoheshimu na kulinda uhuru wa vyombo vya habari.
Wakati wengineo wakitembeza mabakuli ya michango, CCM ilikuwa inaeleza sera, mikakati, mipango ya kimaendeleo kwa Wananchi endapo wataichagua tena Oktoba 28, 2020.
Kwa mtaji wa Watu, sera, rasilimali fedha na haiba ya Wagombea kuanzia ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani CCM inayo nafasi kubwa ya kushinda kwa kishindo uchaguzi huu Mkuu 2020.
Narudia tena kumpongeza Dkt. Magufuli kwa kunadi vyema ilani ya uchaguzi 2020 – 2025 na kuongoza mkutano wa kistaarabu usiokuwa na jazba, matusi wala kashfa.
Pia pongezi kwa Watanzania wote wapenda maendeleo na amani kwa kuendelea kuiunga mkono CCM na kuhaidi kuichagua tena CCM.
Mungu mbariki Dkt. Magufuli
Mungu mbariki Dkt Hussein Mwinyi
Mungu ibariki CCM
Mungu ibariki Tanzania