Mjumbe wa Baraza la TCRA CCC Isaack Mruma akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo |
Mwenyekiti
wa Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Tanga
Christopher Kiemi akieleza jambo wakati mkutano huo kushoto ni Mjumbe wa Baraza la TCRA CCC Isaack Mruma
Katibu wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Masiliano nchini (TCRA CCC) Mkoani Tanga Lulu George akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo |
Sehemu ya wadau wa mkutano huo wakifuatilia matukio mbalimbali kwa umakini
BARAZA
la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Masiliano nchini (TCRA CCC) limeeleza kwamba
huduma ya Pesa Mtandao kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu imepanda kutoka
akaunti milioni 17.4 mwaka 2015 hadi kufikia akautini milioni 28 Mei mwaka
2020.
Hayo
yalisemwa leo na Mkuu wa Idara ya Elimu na Uhamasishaji wa Baraza la Ushauri la
Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano nchini (TCRA CCC) Hilary Tesha wakati wa mkutano
wao na wadau kutoka makundi ya watu wenye mahitaji maalumu Jijini Tanga.
Alisema
huo ni utaratibu wao kama baraza kukutana na makundi tofauti tofauti na mpaka
sasa wana kamati 12 hapa nchini ambazo wanafanya nao kazi ikiwemo ya mkoa wa
Tanga, na mikoa mingine dhumuni likiwa ni kuhakikisha wanawafikia watu wengi
kadri ya uwezo wao.
Tesha
alisema pia mpaka sasa laini za simu zilizotolewa zimeongezeka kutoka milioni
39 hadi mwezi Machi mwaka huu ni milioni 48.9 kwa sasa huku akieleza kwaamba kuna
uwekezano mkubwa zikawa zimeongezeka
“Lakini
pia miamala ya kifedha iliyofanyika kuanzia 2015 hadi Mei mwaka huu imeongezeka
kutoka miamala milioni 131.6 hadi milioni 257.4 hiyo inaonyesha namna watu
wanavyotumia fedha mtandao ya simu za mkononi kuweka fedha kuanzia desemba 2015
hadi machi 2020”Alisema
Awali
akizungumza wakati wa mkutano huo Mjumbe wa Baraza la TCRA CCC Isaack Mruma
alisema kwamba watu wenye mahitaji maalumu alisema kwenye baraza la ushauri na
wasilimia wanataka kuanzia mchakato wa kutunga kanuni maalumu za kuwawaezesha
watu wenye ulemavu waweze kupata haki ya kupata habari.
Alisema
kwa mfano kanuni zipo wazi za kulinda watumiaji za mwaka 2018, kanuni za
maudhui za Radio na TV mwaka 2018 ambazo zimeboreshwa hivi karibuni mwaka huu
na kanuni za maudhui ya mtandaoni iliyoboreshwa zinavipengele kamili vinavyolenga
namna gani watoa huduma za mawasiliano waweze kuwahudumia watu walemavu.
Naye
kwa upande wake Katibu wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Masiliano
nchini (TCRA CCC) Mkoani Tanga Lulu George alisema kwamba harakati za kutetea
haki za watumiaji zilianza mwaka 1960 huku nchini Marekani.
Alisema
mwaka 1962 Rais wa Marekani John Kenedy alitangaza rasmi haki nne za watumiaji
wa huduma za bidhaa ikiwemo haki ya kupata huduma ya mawasiliano.