Home Mchanganyiko WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA WACHANGIA MILIONI 30 UJENZI WA...

WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA WACHANGIA MILIONI 30 UJENZI WA MSIKITI CHAMWINO

0

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na wakuu wa mikoa katika hafla ya kukabidhi mchango kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.

PIX1.Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akizungumza 
wakati wa hafla ya kukabidhi mchango wa shilingi milioni 30 zilizotolewa na Wakuu wa
Vyombo vya Ulinzi na usalama kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa Wilaya ya Chamwino
jijini Dodoma. 

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akimkabidhi Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge mchango wa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma unaojengwa na SUMA JKT ambaye ni mkandarasi wa mradi huo.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Charles Mbuge akizungumza wakati wa hafla ya kupokea mchango wa Wakuu Vyombo vya Ulinzi na Usalama waliochangia milioni 30 na Wakuu wa Mikoa ambao wamechangia shilingi Milioni 26 katika ujenzi wa msikiti wa Wilaya ya Chamwino jijini  Dodoma 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaristi Ndikilo akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Wilaya Chamwino jijini  Dodoma.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Charles Mbuge akikabidhiwa mchango wa shilingi milioni 26 na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaristi Ndikilo  kwa niaba ya wakuu wa mikoa wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Wilaya Chamwino jijini  Dodoma.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Charles Mbuge akikabidhi mchango uliochangwa na Kanisa la AIC Simiyu, na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Wilaya Chamwino jijini  Dodoma.

Sehemu ya Wakuu wa Mikoa walishiriki katika hafla hiyo wakifuatilia hotuba ya
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo kabla hajakabidhi
mchango wa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwezesha ujenzi wa Msikiti wa
Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Shehe wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Bw. Suleiman Matitu akitoa neno la shukrani kwa Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na Wakuu wa Mikoa waliochangia katika ujenzi wa msikiti wa Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma

………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Kias cha Sh.Milioni 68 kimechangwa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini, wakuu wa mikoa na Kanisa la AIC mkoani Simiyu kwa ajili ya kuunga mkono uamuzi wa Rais, Dk. John Magufuli wa kujenga Msikiti wa kisasa na bora eneo la Chamwino jijini Dodoma
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini,Jenerali Venance Mabeyo ameeleza kuwa , wameguswa na uamuzi huo wa kutaka kujenga Msikiti bora na wa kisasa katika eneo hilo.
Aidha awali kabla ya kukabidhi mchango wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Jenerali Mabeyo amesema kuwa kufuatia agizo na uamuzi huo wa la Rais,Dk.Magufuli kutaka kujenga msikiti, aliamua kukaa na wakuu wa vyombo vya ulinzi ambapo walifanikiwa kuchanga kiasi cha Sh. Milioni 30.
“Fedha hizi kiasi cha sh.milioni 30 tulizochanga wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, tumeelekezwa kuzikabidhi kwa mkandarasi wa ujenzi wa Msikiti huu, si mwingine ni Jeshi la kujenga Taifa(JKT), na sasa namkabidhi mkuu wake, Meja Jenerali, Charles Mbuge kwa utekelezaji,”amesema.
Lakini pia wakuu wa Idara za vyombo vya ulinzi na usalama nao walihamasika katika Jambo hilo na wamechanga kiasi cha Sh milioni 10 ambazo atazikabidhi wakati wowote kuanzia sasa kwa mkandarasi wa ujenzi ambaye ni Jeshi la kujenga Taifa(JKT) na kumkabidhi, Meja Jenerali.Mbuge.

Kwa upande wake Meja Jenerali, Munge ameeleza kuwa fedha hizo atahakikisha kazi hiyo inafanyika kwa ukamilifu na kwa wakati huku akiwapongeza wote walijitoa kuchangia na kuunga mkono uamuzi wa rais.

Nao wakuu wa mikoa, wamechangia kiasi Cha Sh. Milioni 26 kwa ajili ya kazi hiyo.

Akizungumza Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa wakati wa kukabidhi mchango huo, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amesema kuwa kufuatia agizo la Rais, Magufuli, wakuu wa mikoa waliguswa na kuamua kutoa kiasi hicho cha fedha ili kuwezesha kazi ya ujenzi wa msikiti.

Akikabidhi mchango uliochangwa na Kanisa la AIC Simiyu, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, aamesema Kanisa limeona ni vyema kuunga mkono juhudi za rais kwa kuchangia fedha hizo.

Naye Sheikh wa Wilaya ya Chamwino, Suleiman Matitu,ametoa shukrani kwa viongozi hao kwa mchango wao amesema, uongozi wa msikiti Wilaya ya Chamwino, wanamshukuru Rais. Magufuli kwa kufanya jambo hilo bila kubagua dini.

“Msikiti huu inatarajiwa kunufaisha kaya zaidi ya 500 zilizopo katika Wilaya hii, pia wageni watakaowasili Chamwino Ikulu, tunashukuru sana, kwa kuwa rais ndiye muanzilishi wa Jambo na mchakato huu,”amesema.

Aidha, Sheikh Matitu aliwashukuru Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Wakuu
wa mikoa kwa kuchangia ujenzi wa msikiti huo.