Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta tayari yupo Birmingham na timu yake, Aston Villa wakijiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya England. Aston Vlla iliyonusurika kushuka daraja msimu uliopita, msimu ujao itaanza na Sheffield United Septemba 19 Uwanja wa Villa Park