Mwanariadha Damian Christian wa Arusha (kulia) ambaye alishika nafasi ya kwanza akiwaongoza wanariadha wenzake kumaliza mbio za mita 800 katika fainali zilizofanyika leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.
Wanariadha Lucia Nestory (kulia) na mwenzake Salima Mussa wote kutoka Mwanza wakimaliza mbio za mita 800 katika fainali iliyofanyika leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara
Msichana Shija Donard wa Mwanza (kushoto) akifuatiwa na Bertha Doto wa Geita, na Emiliana Ndele wa Mbeya kwenye fainali za mita 200 zilizofanyika leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara
………………….
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Wanariadha Damian Christian wa Arusha na Lucia Nestory wa Mwanza wamefanikiwa kushinda fainali za mbio za mita 800 kwa wavulana na wasichana katika mashindano ya UMITASHUMTA yaliyofanyika leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.
Damian alitumia dakika 2:05:11 kujishindia medali ya dhahabu katika fainali hizo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na mkimbiaji Tilulu masanja kutoka mkoa wa Morogoro ambaye alitumia dakika 2:05:32, huku mshindi wa tatu katika mbio hizo akiwa ni Masanja Ngado kutoka mkoa wa Tabora ambaye alitumia dakika 2:05:41 na hivyo kufanikiwa kushinda medali ya shaba.
Kwa upande wa wasichana Lucia wa Mwanza aliyejishindia medali ya dhahabu alitumia dakika 2:21:00, ambapo nafasi ya pili pia ilichukuliwa Salima Mussa pia kutoka Mwanza ambaye alitumia dakika 2:21:16, na nafasi ya tatu ilishikwa na Nyanzobe Mrahi kutoka mkoa wa Mara ambaye alitumia dakika 2: 22:80
Katika fainali za mita 200 kwa wavulana ambazo pia zilifanyika leo asubuhi, nafasi ya kwanza ilishikwa na mkimbiaji Steven Stephano wa Tabora ambaye alitumia muda wa sekunde 24:58 na hivyo kujitwalia medali ya dhahabu, nafasi ya pili ilichukuliwa na mwanariadha Hamis Hussein wa Geita aliyetumia muda wa sekunde 24:97, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Daniel Emanuel wa Mwanza aliyetumia dakika 25:09.
Kwa wasichana, nafasi ya kwanza katika mbio za mita 200 ilichukuliwa na Shija Donard wa Mwanza ambaye alikimbia kwa muda wa sekunde 27:94, nafasi ya pili ilishikwa na Bertha Doto wa Geita aliyetumia sekunde 28:40, na nafasi ya tatu ilienda kwa mwanariadha Emiliana Ndele wa Mbeya ambaye alitumia sekunde 28:45.
Katika fainali za mbio za kupokezana kijiti mita 100 x 4 kwa wavulana nafasi ya kwanza imechukuliwa na mkoa wa Mwanza ambapo washiriki wake walitumia jumla ya sekunde 47:94, nafasi ya pili imechukuliwa na mkoa wa Tabora ambapo wanariadha wake walitumia sekunde 50:19, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na washiriki kutokamkoa wa Mara ambapo walitumia sekunde 51:00.
Kwa wasichana nafasi ya kwanza ilichukuliwa na washiriki wa mkoa wa Mwanza, wakifuatia na mkoa wa Mara na nafasi ya tatu imeshikwa na mkoa wa Geita. Wanariadha wa Mwanza walitumia jumla ya sekunde 54:78, Mara walitumia sekunde 55:15 na Geita walitumia sekunde 57:25.
Katika mashindano ya kuruka chini kwa wavulana nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mwanariadha Laurent Robert wa mkoa wa Geita ambaye alijishindia medali ya dhahabu baada ya kuruka urefu wa mita 5 na sentimita 57, nafasi ya pili ikienda mkoa wa Mwanza ambapo mwanariadha wake Kamdi Momona aliruka urefu wa mita 5 na sentimita 50, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Leonard Vises kutoka mkoa wa Shinyanga ambaye aliruka urefu wa mita 5 na sentimita 47.
Kwa upande wa wasichana katika mchezo wa kuruka chini nafasi ya kwanza ilinyakuliwa na Mosha Julius wa Mwanza ambaye aliruka urefu wa mita 4 na sentimita 57, nafasi ya pili ilichukuliwa Eliza Keraju kutoka mkoa wa Mara ambaye aliruka urefu wa mita 4 na sentimita 42, huku nafasi ya tatu ilichukuliwa na Shija Donard ambaye aliruka urefu wa mita 4 na sentimita 42.
Katika mchezo wa kurusha kisahani kwa upande wa wavulana, nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Kelvin John kutoka mkoa wa Mara ambaye alitwaa medali ya dhahabu aliyefanikiwa kurusha umbali wa mita 25 na sentimita 98, nafasi ya pili ikichukuliwa na Sadiki Mgale wa Songwe ambaye alirusha umbali wa mita 23na sentimita 73 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Njendage Njanje wa Manyara aliyerusha umbali wa mita 23 na sentimita 23.
Kwa wasichana, mshindi wa kwanza ni Debora Dambela wa Manyara ambaye alirusha kisahani umbali wa mita 20 na sentimita 46, nafasi ya pili ilichukuliwa na Mariam kumge wa Simiyu ambaye alirusha umbali wa mita 19 na sentimita 62, huku nafasi ya tatu ilichukuliwa na Shija Donard wa Mwanza ambaye alirusha umbali wa mita 19 na sentimita 59.