Mgeni Rasmi kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya Bukoba Msela Bumbuli kulia akikatata utepe na Bw. George Leo kushoto kuashiri kukamilika kwa makabidhiano ya jengo la mama na mtoto lililojengea na shirika la World Vision Mradi wa Rukoma A P kituo cha afya Rubale. George Leo aliyesimama akitoa taarifa ya Mradi wa Rukoma A P kwa mgeni rasmi na wanachi waliohudhuria kwenye hafla ya makabidhiano ya wodi ya mama na mtoto kituo cha afya Rubale kwaniaba ya meneja wa shirika la World Vision kanda ya Kagera.
Mwonekano wa jengo la wodi ya mama na mtoto kituo cha afya Rubale lililojengwa na shirika la World Vision Tanzania kwa mradi wa Rukoma A P likiwa limegharimu kiasi cha shiri milioni 118 fedha za kitanzania hadi kukamilika kwake.
Mratibu wa mradi wa Rukoma A P Bw. Lugembe Ng’oga akitoa maelezo kwa mgeni rasmi pamoja na wananchi juu ujenzi wa jengo la mama na mtoto kituo cha afya Rubale kwa ndani na matumizi yake.
Wananchi pamoja na wahudumu wa kituo cha afya wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi Msela Bumbuli watatu kutoka kushoto pamoja na watumishi wa shirika la world vision baada ya makabidhiano ya jengo la wodi ya mama na mtoto kituo cha afya Rubale.
***************************************
Na Allawi Kaboyo Bukoba.
Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision Tanzania limekabidhi jengo la wodi ya Mama na Mtoto ikiwa ni moja ya ahadi walioitoa katika kituo cha afya Rubale baada ya kuwepo kwa changamoto hiyo kwa wakina mama wajawazito kwa kipindi kirefu.
Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika Agosti 18, Mwaka huu katika kituo cha Afya Rubale halmashauri ya wilaya Bukoba Mkoani Kagera na kuhudhuriwa na baadhi ya wananchi wanaotumia kituo hicho pamoja na uongozi wa kijiji cha Rubale.
Akiongea kabla ya kukabidhi jingo hilo kwa niaba ya Meneja wa shirika hilo kanda ya Kagera Bw. George Leo amesema kuwa shirika hilo limekuwa likitekeleza miradi mbalimbali hapa nchini na kwaupnade wa Mradi wa Rukoma A P wamejenga vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali, wametengeneza madawati, wamejenga vyoo, nyumba ya mwalimu na wodi ya mama na mtoto.
Bwana Leo amesema kuwa Mradi wa Rukoma A P ulianza kutekelezwa kuanzia mwaka 2016 ambapo mpaka mwaka huu wanajivunia kufanikisha baadhi ya miradi walioitekeleza huku mradi wa wodi ya mama na mtoto kituo cha afya rubale ambayo hadi kukamilika kwake imetumia kiasi cha shilingi milioni 118 fedha za kitanzania.
“Shirika letu linalenga sana kumuhudumia mtoto, na sisi katika kuhakikisha mtoto anakuwa salama tanajitahidi kuboresha miundombinu kama kuboresha upande wa kumpatia elimu mtoto iliyo bora, Afya ya mtoto, lishe na maji safi na salama. Kituo hiki kilikuwa zahanati na baadae kupandishwa hadhi ya kuwa kituo cha afya hali hiyo ilipelkea watoto na watu wazima kulazwa katika wodi moja na hilo ndilo lililotupelekea sisi kuomba ufadhiri wa kujenga wodi hii.”
Ameongeza kuwa jingo hilo tayari limekamilika ambapo ameiomba serikali kuhakikisha inamalizia masuala ya upatikanaji wa maji, vifaa tiba, wahudumu na kuliwahsa umeme ili lianze kutumika kwa wananchi kwa lengo lililokusudiwa huku akiwaomba wananchi kulitunza jingo hilo.
Kwaupande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya Bukoba, akiongea kwaniaba ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo amelishukuru shirika la World Vision kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuwajali wanyonge kwa kuwaboreshea maisha.
Amesema kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo kwenye jamii itasaidia kuinua uchumi kwa kuwa maisha sasa yatakuwa rahisi, kwa upande wa afya watakuwa wanapata huduma bora na sahihi na kuongeza kuwa jingo lililojengwa linakidhi mahitaji na kuahidi kulitunza kwa maslahi ya wananchi.
Aidha Bumbuli amesema kuwa changamoto zilizobakia serikali itahakikisha inazimaliza kama maji umeme, vifaa tiba na wahudumu wa afya ambalo hilo amesema ni jukumu la serikali ili kuhakikisha malengo ya jingo hilo yanatimia huku akizidi kuliomba shirika kuendelea kuisaidia serikali.
Creophas Bugingo ni mwenyekiti wa kijiji Rubale ameshukuru shirika kwa kuwapatia jengo hilo ambalo litatoa fursa kwa wanawake wajawazito kujifungua kwa usalama huku mganga mfawidhi wa kituo hicho Daktari Tuvatus Madio amesama kuwa ujio wa kituo hicho utasaidia utoaji wa huduma kuboreka na kitasaidia wodi iliyokuwa ikitumika kama wodi ya wanawake itatumika kwaajili ya wanaume maana hapo awali wodi ya wanaume haikuwepo.
Baadhi ya wakina mama waliohudhuria hafla hiyo wakiongea kwa furaha ya kupata jingo hilo wameeleza adha walizokuwa wakizipata hapo awali kuwa walikuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kwenda hospitali Teule ya Izimbya ili kujifungua kwa usalama.
Wamesema kuwa walikuwa wakidhalilika sana kwa kukosa jingo la mama na mtoto na wengine kupelekea kujifungulia barabarani kwa kukosa msaada wa haraka na stara ya kiubinadamu.
Kituo cha afya Rubale nje ya kutokuwa na wodi maalumu ya wanaume kinachangamoto ya chanzo sahihi cha maji cha kudumu maaana hutegemea maji ya mvua hali inayowapelekea wanaopata huduma kituoni hapo kuadhirika pamoja na jiko kwaajili ya wanaowahudumia wagonjwa pamoja na upungufu wa watumishi huku waliopo wakiwa 13.