Home Mchanganyiko MWADIMA-VIJANA WAJITOKEZE KUSOMA MASOMO YA UTALII KAMA ILIVYO MASOMO YA UFUNDI NA...

MWADIMA-VIJANA WAJITOKEZE KUSOMA MASOMO YA UTALII KAMA ILIVYO MASOMO YA UFUNDI NA MENGINE

0

***************************

NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
KUNDI la Vijana,wametakiwa kujitokeza kusomea masomo ya Utalii ili kuinua sekta hiyo,  ambayo awali ilionekana kama kazi ya watu wasiosoma.
Hatua hiyo inayolenga kuboresha soko la Utalii nchini ambalo lina nafasi kubwa katika kuboresha sekta uchumi kupitia utalii, kwa walengwa hao kuingia kisha kutembelea maeneo mbalimbali yenye vivutio ikiwemo katika mahoteli makubwa kila kukicha.
Rai hiyo imetokela na Meneja wa Hoteli ya Kitalii ya Oceanic Bay ya mjini Bagamoyo David Mwadima, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, ambapo alisema umefika wakati sasa kwa wa- Tanzania kujikita katika masomo ya Utalii.
“Hapa tuna vijana wengi wanatokea mikoa mbalimbali nchini wapo Oceanic Bay kwa ajili ya kusomea sekta ha Utalii,  niwaase wazaze wawasomeshe watoto wao,” alisema Mwadima.
Aliongeza kuwa hivi karibuni soko hilo liliyumba kidogo kutokana na ugonjwa wa Corona,watalii walishindwa kufika kutokana na nchini zao kuwazuia raia wake kutoka au kuingia, hali iliyochangia kushuka kwa biashara lakini sasa biashara inaanza kurejea vizuri.
Kwa upande wake Mhandisi Ndikilo aliupongeza uongozi huo, na akiwaasa wasilewe sifa badala yake waongeze bidii ya kuwahudumia wateja wao.
Ndikilo alibainisha ,kwa mkoa wa Pwani sekta hiyo inakua kutokana na watalii mbalimbali kuingia mkoani hapo kwa kutembelea vivutio na mbuga ya selou ,saadan na nyingine hali inayowezesha kuinua pato na mkoa na nchi kijumla.