…………………………………………………………………………..
Taasisi ya Tulia Trust imetoa msaada wa mifuko 140 ya Cement katika Shule ya Msingi Halinji na Nsalaga zilizopo jijini Mbeya ili kusaidia ujenzi wa madarasa unaoendelea katika shule hizo, akikabidhi msaada huo Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amewataka Wananchi wajue kutofautisha misaada inayotolewa na taasisi hiyo na mambo ya siasa.
”Kuna watu huwa wanachanganya mambo, tuwekane vizuri hapa ili mtu asije kurudi nyumbani akiumwa na pressure. Ndugu zangu muda wa kampeni bado na mimi hapa sijaja kama mgombea bali nimekuja kama kiongozi wa taasisi inayoitwa Tulia Trust” amesema -Dkt. Ackson
“Tulia Trust huwa inakuja huku wakati wote sio leo tu na mara nyingi sio lazima mimi niwepo lakini leo nimekuja mwenyewe, nimeona nifafanue hilo maana hapa kuna watu wataanza kuchanganya mambo. Muda wa kampeni bado na hadi sasa wagombea hawajateuliwa kwahiyo kila mmoja awe na amani” -Dkt. Tulia Ackson
“Tunapotoa hii michango sio kwamba tunauwezo sana, hapana. Niwaombe sana wananchi, sisi kama jamii yule mwenye kauwezo kidogo tuendelee kujitoa katika michango mbalimbali pale inapobidi ili kuweza kuwawezesha watoto wetu kusoma katika mazingira mazuri maana hatujui huwenda hata Rais ajaye anaweza kutoka kwenye hizi shule”-Dkt. Tulia Ackson