KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemtangaza winga Mghana, Bernard Morrison kuwa mchezaji huru baada ya kubaini mkataba wake na klabu ya Yanga ulikuwa una mapungufu.
Baada ya shauri lililosikilizwa kwa siku tatu mfululizo kuanza juzi, hatimaye leo jioni Mwenyekiti Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, Wakili Elias Mwanjala amesema;
“Malalamiko, kesi iliyoletwa kwetu na Bernard Morrison kusema kwamba yeye hakusaini mkataba wa wa kuongeza muda na Yanga, kwa hiyo tumeangalia vitu vingi, kimsingi tumegundua kwamba mkataba una walakini kidogo, kwa hiyo tumempa faida Morrison, kwa maana ya kwamba tumeona kwamba Yanga wana mkataba ambao ulikuwa una utata kidogo,”.

Pamoja na hayo, Wakili Mwanjala amesema Morrison atapelekwa Kamati ya Maadili kwa kitendo cha kusaini mkataba wa Simba wakati shauri lake halijatolewa hukumu.
Tayari Morisson amekwishatambulisha kuwa mchezaji mpya wa mahasimu, Simba SC baada ya miezi sita ya kuwatumikia Yanga SC akitokea kwao, Ghana.