Home Mchanganyiko MHE.KADIO AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA WANADHIMU NA WAHASIBU KUTOKA MAKAO MAKUU...

MHE.KADIO AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA WANADHIMU NA WAHASIBU KUTOKA MAKAO MAKUU YA POLISI

0

*********************************

Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi amefungua kikao kazi cha Maafisa wanadhimu na wahasibu kutoka makao makuu ya Polisi, Mikoa na Vikosi Tanzania Bara na Visiwani. Kikao kazi hicho ni cha siku mbili kuanzia leo tarehe 12/08/2020 hadi tarehe 13/08/2020 kinachofanyika katika ukumbi wa Shule ya Polisi Tanzania – Moshi (CCP), kikiwa na kaulimbiu inayosema “UADILIFU KATIKA USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA HUCHAGIZA MAENDELEO “

Katika hotuba yake ya ufunguzi amewataka washiriki kushiriki kikamilifu katika kujadili changamoto zilizopo katika ukusanyaji wa maduhuli ya serikali na kuzipatia ufumbuzi. Aidha amewataka kila mmoja kwa nafasi yake kuacha alama kwa kuleta mabadiliko chanya katika eneo lake la kazi ili serikali iweze kunufaika na uwepo wake.

Pia amesisitiza swala la kuwa na weledi na uadilifu wa hali ya juu, uwajibikaji, Usiri na kuweka mazingira mazuri ya kila mmoja kuwa muadilifu katika kusimamia mali za umma.

Amewapongeza washiriki na Jeshi la Polisi kwa ujumla kwa kufanikiwa kuwatumia wataalamu wake wa ndani na kufanikiwa kutengeneza mfumo wa ukusanyaji wa maduhuri ya serikali.

Kabla ya Katibu Mkuu kutoa hotuba yake ya ufunguzi kaimu kamishina wa fedha na lojistiki Naibu kamishina KIDAVASHARI ambaye alimwakilisha Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania katika kikao hicho alisema washiriki watapata nafasi ya kujadili changamoto zilizopo katika usimamizi wa rasilimali fedha ndani ya Jeshi la Polisi.

Aidha alieleza katika kikao hicho watapata fursa ya kupata mada inayohusiana na mabadiliko ya mifumo ya usimamizi wa fedha, pia mabadiliko ya mfumo wa ulipwaji wa fedha za serikali na mada nyingine mbalimbali za kuwajengea uwezo na ufanisi washiriki katika kutekeleza majukumu yao.

Katibu Mkuu katika kuhitimisha hotuba yake aliwataka maafisa wanadhimu na Jeshi la Polisi kwa ujumla kuhakikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28/10/2020 wanatekeleza jukumu lao la kulinda maisha ya watu na mali zao kwa weledi na kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika katika mazingira ya amani na utulivu, bila kujali swala la dini, kabila au itikadi za vyama badala yakewazingatie sheria.