Waziri wa Ardhi nyumba na Makazi Mh.Willam Lukuvi akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati alipotoa taarifa ya kufuta umiliki wa mashamba ya kijiji cha Kazole wilayani Mkuranga yaliyokuwa yakimilikiwa na kampuni ya Soap and Allied Industries kuanzia Oktoba 1988 kwa miliki ya miaka 99 kwa matumizi ya kilimo na ufugaji.
………………………………………
Waziri wa Ardhi nyumba na Makazi Mh.Willam Lukuvi amefuta Hati miliki ya jumla ya karibu 4222 ya mashamba yaliyokuwa zikimilikiwa na wawekezaji wawili tofauti katika wilaya ya Mkuranga baada ya kushindwa kuziendeleza na kisha kuibua mgogoro na wananchi.
Shamba la kwanza ekari 2472 lililopo eneo la Luzando awali kabla ya kufata umiliki wake ,lilikuwa likimilikiwa na wawekezaji wawili Abdulsulatan Ali Jesa na Hassanali Jesa kuanzia miaka ya 1951 kwa matumizi ya kilimo na baadae kulihamishia umiliki wake kwa wawekezaji wengine ambao ni Emtiyaz Rajwan na Karim Manji.
Shamba jingine ekari 1750 lililopo eneo llililopo kijiji cha Kazole lilikuwa likimilikiwa na kampuni ya Soap and Allied Industries kuanzia Oktoba 1988 kwa miliki ya miaka 99 kwa matumizi ya kilimo na ufugaji.
Hata hivyo pamoja na umiliki wa ekari 2472 aa kijiji cha Lusando , umiliki wake kwa mwekezaji huyo ulilalamikiwa baada ya uwepo wa madai kuwa kabla ya kumilikishwa kulikuwa na vijiji vinne ndani yake vinavyokaliwa na watu.
Hatua hiyo imetokana na malalamiko yaliyoibuliwa wiki iliyopita na mmoja wa wananchi wakati Rais John Magufuli aliposimama kuwasilimia wakati ukitoka Lupaso mkoani Mtwara katika maziko ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa.
Akitoa uamuzi huo leo Waziri William Lukuvi pamoja na kuwalalamikia viongozi wa Wilaya ya Mkuranga kutokana na uwepo wa dalili za rushwa katika kulishughulikia suala hilo, aliagiza baadhi ya maeneo hayo kugawiwa kwa wananchi waliopo katika maeneo hayo na mengine kurejeshwa Serikalini ili kupangiwa utaratibu mwingine.
“Huwezi kumiliki ardhi tena yenye watu wanaoishi ndani yake, kufanya hivyo ni sawa na kununuu ardhi hiyo pamoja na wananchi waliopo ndani yake, hii ndiyo kazi ya Serikali ya awamu ya tano kutetea haki za wanyonge” alisema Lukuvi
Amesema Lukuvi mbele ya wawekezaji hao pamoja na viongozi wa wilaya hiyo wakati akizungumza na wananchi, Waziri Lukuvi amesema Serikali ya Rais Magufuli haipo tayari kuona wananchi wake wakinyanyasika katika ardhi yao tena kwa kuchukuliwa na wawekezaji ambao hata hivyo wamekiuka taratibu za uwekezaji.
Aidha Waziri Lukuvi aliwataka wawekezaji hao kwa kurejesha hati za umiliki wa ardhi hiyo pamoja na kufuata kesi walizozifungua mahakamani kama kweli wana nia njema na matakwa yao ya kumiliki tena ardhi kwa majibu wa sheria.
Suala la mgogoro wa ardhi hiyo kimsingi lilichukua mgogoro kwa kipindi kirefu hadi kupelekea wananchi wa vijiji hivyo kwa pamoja na wawekezaji hao kufungua kesi kwa nyakati tofauti mahakamani.
Waziri wa Ardhi nyumba na Makazi Mh.Willam Lukuvi akizungumza na Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mkuranga Bw. Abdalla Ulega katika mkutano wa hadhara wakati alipotoa taarifa ya kufuta umiliki wa mashamba ya kijiji cha Kazole wilayani Mkuranga yaliyokuwa yakimilikiwa na kampuni ya Soap and Allied Industries
Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mkuranga Bw. Abdalla Ulega akizungumza katika katika mkutano wa hadhara wakati Waziri wa Ardhi nyumba na Makazi Mh.Willam Lukuvi alipotoa taarifa ya kufuta umiliki wa mashamba ya kijiji cha Kazole wilayani Mkuranga yaliyokuwa yakimilikiwa na kampuni ya Soap and Allied Industrie.
Waziri wa Ardhi nyumba na Makazi Mh.Willam Lukuvi akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga kushoto ni Mkurugenzi wa wilaya ya Mkuranga Bw. Mshamu Ally Munde.
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Ardhi, Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga na Mkoa wa Pwani pamoja na maofisa wa halmashauri hiyo wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wakifurahia uamuzi wa serikali kufuta mashamba hayo na kuyarudisha kwa halmashauri ya Mkuranga kwa matumizi menginya makazi.
Waziri wa Ardhi nyumba na Makazi Mh.Willam Lukuvi akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga kushoto ni Mkurugenzi wa wilaya ya Mkuranga Bw. Mshamu Ally Munde pamoja na viongzo wengine wakikagua mashamba hayo.