Mkurugenzi wa Biashara TTCL, Bw.Vedastus Mwita akizungumza na Wanahabari katika ofisi za Kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam Meneja wa Bidhaa TTCL, Bw.John Yahaya akizungumza leo na Wanahabari katika Ofisi za Kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam.
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wateja wapya wa Mtandao wa TTCL hapa nchi kunufaika na promotion mpya ambayo imezinduliwa hii leo ya KARIBU NYUMBANI PROMO ambayo itamrahisishia mteja wa huduma hiyo kupata huduma za mawasiliano kwa nafuu zaidi.
Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara Bw.Vedastus Mwita amesema promotion hiyo inaenda kuwapatia watumiaji wa huduma zao vitu mbalimbali vya msingi ambavyo vitatia chachu katika kutumia huduma zao hasa baada yakuwa Watanzania wamewaunga mkono na kurudi nyumbani kwa wingi.
“Katika Promotion yetu ya KARIBU NYUMBANI PROMO kwanza tutakuwa na promotion ambayo itahusu watumiaji wa simu za mkononi, promotion hii ni kwa wateja wapya wote wa TTCL ambapo watajiunga na huduma zetu kuanzia hivi leo tarehe 04 mwezi 08.
Aidha Bw.Mwita amesema wateja wote watakaojiunga katika huduma za TTCL za simu ya mkononi watapata laini bure pia watapata dakika 30, MB 100 na Sms100 ambazo zitatumika ndani ya ya siku 7 na zitaenda katika mitandao yote.
“Ili mteja kuweza kunufaika na huduma hii au promotion hii kwa wale watumiaji wa simu za mkononi basi atahitajika tu kuweka Tsh.1,000/= katika laini yake. Hii pesa ambayo anaiweka mteja si kwamba itatumika kwaajili ya huduma hizi ambazo nimzisema nikimaanisha dakika 30, sms 100 na MB 100 hapana itaendelea kuwepo na atapata pia nyongeza hii”. Amesema Bw.Mwita.
Hivyo basi Bw.Mwita amesema kuwa huo ni muendelezo wa kunogesha huduma zao wanazozitoa kwa wateja wao na wanapenda kuwaambia Watanzania kwamba wazidi kurudi nyumbani ili kunufaika na promotion hii maalumu ambayo inaanza hivi leo.
Pamoja na hayo Bw.Mwita amesema promotion hiyo pia itagusa watumiaji wa huduma za simu za ofisi ama mezani kwani wameondoa gharama za uunganishaji wa huduma hizo.
“Kuanzia leo kuunganishwa na huduma hizi ni bure lakini mbali na kuwa sasa ni bure wateja wetu wataenda kunufaika kwani kila atakaejiunga atapata dakika 100 za kupiga simu kwenda mitandao yoyote au kuwasiliana kwa kutumia zile huduma zetu za fixed na dakika hizo zitatumika ndani ya siku 30. Mbali na hapo atapata MB 4 ambazo pia atazitumia ndani ya siku 30”. Amesema Bw.Mwita.
Nae Meneja wa bidhaa, Bw.John Yahaya amesema wanapenda kuwahamasisha Watanzania waweze kurudi nyumbani waweze kutumia huduma za TTCL kwani huduma hizo ni uhakika na zinakupa kile ambacho unakihitaji katika mawasiliano.